Like Us On Facebook

AFYA......FAIDA ZA JUISI YA UKWAJU.

Tunda  la  Ukwaju. Tunda  la ukwaju  ni  tunda  lenye  faida  nyingi  sana  kwa  afya  ya  mwanadamu. Tunda  hili  huweza  kutumika  kutengeneza  juisi  ambayo  matumizi  yake   yana  faida  kubwa  sana  katika  afya  ya  mwili  wa  mwanadamu.


                                                             Juisi  ya  Ukwaju.
                    NAMNA  YA  KUTENGENEZA  JUISI  YA  UKWAJU.

Nunua  ukwaju  wako, ukwaju  unapatikana  kwa  wingi  sana  masokoni  na kwenye  supermarkets

  • andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu 
  • baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni 
  • uache uchemke  kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu 
  • ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe 
  • andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
  • weka sukari kwa kiasi unachopendelea 
  • pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste 
  • weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa .
  •  FAIDA   YA  JUISI  YA  UKWAJU.


    1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
    2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
    3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
    4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
    5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
    6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
    7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
    8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
    9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
    10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

    NB: Ikiwa ukwaju na asali havikudhuru, basi changanya hivyo viwili ili kupata faida maradufu!
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari