MWANAFUNZI
wa kike,miaka 13, (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la tano katika
shule ya Msingi Unyakumi, mkoani Singida, amefanyiwa unyama kwa kubakwa
na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Mapunda ambaye ni dereva wa
bodaboda.
Denti aliyebakwa akiwa hospitali
Akizungumza
kwa shida kutokana na maumivu makali aliyonayo akiwa katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, denti huyo alisema kwamba mkasa huo ulimpata
Novemba 19, mwaka huu wakati akitoka shule akielekea nyumbami kwao.
Akisimulia mkasa huo mwanafunzi huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Imekufa kwa kuwa nateseka kitandani kwa muda mrefu sasa kutokana na maumivu yaliyotokana na kubakwa.Nimekua wa kujisaidia kitandani, nawakumbuka wazazi wangu, leo hii wangekuwepo wangekua watetezi wagu, sina uhakika kama nitapona na kwenda shule tena.
“Kutoka shuleni hadi nyumbani ni mwendo wa saa moja, siku hiyo niliyobakwa ilikua Ijumaa, nilikua natoka shule nikielekea nyumbani, njiani kuna vichaka na mashamba ya mikorosho, nilipofika karibu na banda bovu nilimkuta kijana amekaa juu ya jiwe.
“Nilijisikia vizuri sana nilipomuona, uoga ulinitoka juu ya wanyama wakali, sikua na hofu ya aina yoyote kama angenigeuka, nilipomkaribia alinikamata kwa nguvu, alinivuta akanipeleka katika banda bovu.
“Nilijaribu kujinaswa lakini nilishindwa kwani alikua na nguvu kuliko mimi, niliamua kupiga kelele ili nipate msaada toka kwa mtu yeyote anayepita, hata hivyo, hakuna aliyejitokeza, alinifunika mdomo, alinipiga, niliishiwa nguvu, akaniingilia, alipomaliza haja yake, akakimbilia pasipojulikana.
“Nilitokwa damu nyingi zilizotoka sehemu za siri, niliinuka na kutembea kwa shida kwani hata kiuno kilikua kikiuma sana, nilifika nyumbani, sikumkuta dada kwani alikuwa ana kawaida ya kurudi usiku akitokea kazini kwake.
“Aliporudi alikuta nimeshafua nguo zangu na nimeshalala, niliona aibu kumweleza, ilipofika Jumapili maumivu ya kiuno na sehemu za siri yakaongezeka, nilikua nikitembea kwa shida, ilimbidi dada aniulize nina nini? Awali niliogopa kumweleza lakini baadaye nilimsimulia kila kitu kwani maumivu yalizidi.
“Nilishindwa hata kwenda shule, nilipelekwa hosptali ya wilaya lakini hali yangu ilizidi kuwa mbaya. Nikahamishiwa hospitali ya mkoa, Singida lakini sikuweza kupata nafuu, nikaletwa hapa Muhimbili kwa gari la wagonjwa ‘ambulance’ kwani nilishindwa kukaa kwenye kiti cha basi.
“Bado sijaweza kukaa wala kuinuka, hata kulala kwangu ni kifudifudi, nalishwa, naogeshwa kitandani, kwa kweli sina raha hata kidogo tangu nifanyiwe unyama huo maana sijaenda shule, wenzangu wamefanya mitihani mie sipo, nauguza mamivu.
“Nimeoza sehemu za siri hadi makalio, natokwa na usaha, siamini kama nitapona na kwenda shule tena. Aliyenitenda haya tunaishi naye mtaa mmoja na hajawahi kunitongoza ila aliamua kunibaka.
“Nimefikishwa hapa Muhimbili Novemba 20, mwaka huu, naomba taarifa hizi zimfikie mama popote alipo kwani aliachana na baba akarudi kwao Musoma,”alieleza kwa uchungu denti huyo.
Dada wa mtoto huyo anayeishi naye aliyejitambua kwa jina moja la Rose alipoulizwa juu ya madai hayo alikiri kutokea na ameiomba serikali imkamate mtuhumiwa ili haki itendeke.