Mariamu akiugulia maumivu. |
MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya
Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika
kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na
kukatwakatwa mapanga.
Mama huyo aliliambia gazeti hili akiwa
katika Hospitali ya Wilaya Bomani, Tarime kuwa mume wake Marwa Ogora
alimkatakata mapanga baada ya kumtuhumu kuwa akikwenda kwa hawara yake
badala ya kwenda kwenye mazishi ya mjomba wake huko Bunchari.
Akifafanua zaidi, Eliza alikuwa na haya ya
kusema: ‘’Mjomba alifariki na mazishi yake yalifanyika Desemba, kumi na
sita mwaka huu ambapo nilihudhuria baada ya kumwarifu mume wangu kuwa
nitahudhuria lakini alinijibu kuwa hakuwa na fedha za kunipa ili niende
kwenye mazishi.
“Nilichukua jukumu la kwenda kwa
kutumia nauli yangu kwa kuwa muda huo mume wangu alikuwa kazini na baada
ya mazishi kesho yake asubuhi Desemba kumi na saba mwaka huu nilirudi
nyumbani na kumkuta mume wangu ambaye alianza kunipiga kwa mpini wa
jembe kisha panga akidai kuwa sikuwa nimeenda kwenye mazishi badala yake
nilikuwa nimeenda kwa mpenzi wangu.
“Alinishambulia sehemu mbalimbali za
mwili hususani kichwani, kidogo anitoe ubongo, wasingekuwa majirani
kuniokoa baada ya kupiga yowe naamini angeniua kwani hivi sasa siwezi
hata kuamka na masikio yameziba, miguu ina ganzi, siwezi kutembea.
“Mume wangu Ogora amekuwa akinipiga
mara kwa mara lakini kutokana na watoto tuliozaa naye nimekuwa
nikivumilia mateso, naogopa kuondoka na kuacha watoto walelewa na mama
wa kambo,”alidai mama huyo.
Ogora hakupatikana kuzungumzia tukio
hilo kwani anasakwa na dola na afisa mmoja wa polisi wilayani hapa
wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema wanaendelea kumtafuta
mtuhumiwa. Naye daktari wa hospitali aliyolazwa mama huyo, Nega Malico
alikiri kumpokea mgonjwa huy