Like Us On Facebook

BAADA YA LIVERPOOL KUIPA KIPIGO KITAKATIFU ARSENAL,SHABIKI WA ARSENAL NCHINI KENYA AMUUA SHABIKI WA LIVEPOOL KWA KUMCHOMA KISU

MWANAUME mmoja alichomwa  kisu hadi kufa wakati akitazama mechi ya kandanda mjini Meru baada ya kutofautiana na mwenzake kuhusu mechi iliyokuwa ikiendelea.
Marehemu alikuwa akitazama mchuano kati ya timu ya Arsenal na Liverpool wakati walipoanza vita katika baa ya Marete eneo la Makutano.
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Polisi eneo hilo Tom Odero alisema mshukiwa David Mwangi, ambaye ni shabiki wa timu ya Arsenal alimdunga kisu Anthony Muteithia, shabiki wa Liverpool. Bw Odero alisema mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 25 alikufa alipokuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Meru.
“Mshukiwa alilazimika kutoroka lakini wakazi walifanikiwa kupata pikipiki aliyokuwa nayo na kuiwasilisha kwa maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Meru. Msako wa kumkamata umeanzishwa,”alisema Bw Odero.
ars
Mkuu huyo wa polisi alisema uchunguzi umeanzishwa kutambua chanzo cha mzozo wa wawili hao.
Katika mchezo huo Arsenal walichapwa 5-1 na Liverpool.
Credit Swahili hub
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari