Like Us On Facebook

YANGA YAJIOKOTEA KIBONDE YAKIPIGA GOLI SABA KAMA WAMESIMAMA,WAKOMORO HOI TAIFA

http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/02/Screen-Shot-2014-02-08-at-6.15.41-PM.png
Ubao wa Matokeo.
 Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Hamis Kiiza akiipachikia timu yake bao la nne kati ya saba yaliyotiwa kimiani mpaka sasa wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga inaongoza kwa Bao 7-0.
 Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku mabeki wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro wakimsindikiza wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika unaoendelea kuchezwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga imeshinda kwa Bao 7-0.

 Mrisho Ngassa bado yuko na mpiraaaaa.....
 Mrisho Ngassa anapachika bao paleeeee...... Gooooooooo ni goli la sita hili linaungwa hivi sasa na Mrisho Ngassa na kuwa mchezaji pekee aliefunga bao tatu peke yake.
Wachezaji wa timu ya Komorozine wakilaumiana.
 Mshambuliaji wa Pembeni wa Timu ya Yanga,Simon Msuva (27) akiwatoka mabeki wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Mshambuliaji wa Pembeni wa Timu ya Yanga,Simon Msuva (27) akichuana vikali na Beki wa Timu ya Komorozine ya nchini Comoro,Ahmad Houmadi (5) wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Wachezajiwa timu ya Yanga wakishangilia bao lao la pili lililotiwa kimiani na Mchezaji Nadir Haroub.
 Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Haroun Niyonzima akiafanya makeke yake wakati alipotaka kumtoka Beki wa Timu ya Komorozine ya nchini Comoro, Ali Mohamed wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mashabikiwa Timu ya Yanga.
 
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari