KLABU
ya Manchester United inahofia Robin van Persie anaweza kuendelea kuwa
nje kwa wiki sita zaidi baada ya kuumia paja sehemu ile ile aliyowahi
kuumia alipokuwa Arsenal.
David
Moyes anayemuhitaji sana mshambuliaji huyo wake hatari arejee uwanjani
kutokana mwenendo mbaya wa timu hivi sasa, jana Ijumaa amethibitisha
kwamba Wayne Rooney pia anaweza kukosa mechi ya leo dhidi ya Swansea.
Lakini
mtu anayemuumiza kichwa aswa Moyes ni Van Persie, kocha huyo amesema
kwamba hawezi kutaja tarehe ya kurejea uwanjani kwa mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 30, hata baada ya kumpeleka Uholanzi akafanyiwe
kazi na kocha wa viungo wa PSV Eindhoven.
Hasara juu ya hasara: Van Persie anaweza kuwa nje kwa wiki sita zaidi baada ya kuumia paja
Kuna
wasiwasi Van Persie akawa nje kwa muda mrefu zaidi, kwa sababu ameumia
sehemu ile ile ambayo aliwahi kuumia akiwa Arsenal Desemba mwaka 2007 na
akakaa nje kati ya Desemba 16 na Machi 9, akicheza mechi 15 tu.
Mholanzi
huyo hajakitumikia kikosi cha Moyes tangu Desemba 10 na jana kocha wa
United amesema pia kwamba Rooney amepelekwa Misri kwa matibabu sababu ya
hali ya hewa pamoja na maofisa wa dawati la tiba la timu hiyo, ili
aweze kuwahi mechi na Chelsea Januari 19.