Like Us On Facebook

JENGO LA TTCL MAKAO MAKUU DSM LAUNGUA MOTO ASUBUHI YA LEO

                         Jengo la TTCL lenye ghorofa 12 lililoshika moto katika ghorofa ya sita.
 Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kutoka Halmashauri ya jijini likifika katikam eneo la tukio.  
 Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakijiandaa kukabiliana na moto huo.
 Askari wa Kikosi cha Zimamoto akijiandaa kuingia ndani ya ofisi za TTCL zilizoshika moto, hata hivyo kutokana na kuwa na vifaa duni walishindwa kuingia ndani.
 Moto ukiendelea kuwaka katika baadhi ya ofisi.
Magari ya Kikosi cha Zimamoto kutoka Kampuni ya Altimate yalianza kuwasili kwa ajili ya kusaidiana na wenzao wa Kikosi cha Zimamoto kutika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Kituo cha mafuta cha Puma ambacho kipo jirani na jengo la TTCL.


DAR ES SALAAM, Tanzania

Jengo la TTCL, Makao makuu, EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa 1:20.

Moto huo ulikuwa unawake katika ghorofa ya sita ya jengo hilo na ulikuwa unawake katika vyumba vitatu kwa mara moja.

Habari Mseto ilifanikiwa kufika mapema katika jengo hilo na kukuta pilika nyingi za wafanyakazi kuondoa magari yao, na magari ya shirika hilo kongwe nchini.

Magari ya kikosi cha zimamamoto kutoka kikosi cha ukoaji cha Jiji la Dar es Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini kulikuwa na ubishani kati ya wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya wafanyakazi wa Zimamoto kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita kukagua jengo lakini walifukuzwa kama mbwa,
Licha ya Kikosi hicho kuwahi hawakuwa na maji yenye pressure na ngazi za nje kufika hadi ghorofani, hali iliyopelekea watu kutumia ngazi za ndani kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Gari ya Ultimate Security walifika mnamo saa 12:30 na kwa ushirikiano moto uliweza kufanikiwa kuzimwa.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari