Like Us On Facebook

MGOMO WA MADEREVA WA MALORI WAINGIA SIKU YA PILI MIZANI YA KIBAHA,HII NI RIPOTI KAMILI YA MGOMO HUO

 
           Magari yakiwamo malori ya mizigo, mabasi ya abiria na magari mengine yanayosafiri kuelekea mikoani na kuingia Jijini Dar es Salaam, yamekwama kweny foleni kubwa katika Mkoa wa Pwani, kuazia Wilaya ya Kibaha mpaka Mbezi jijini Dar es Salaam baada ya madereba wa malori kudaiwa kufanya mgomo .
Taarifa zinaeleza kwamba madereva wa malori wamegoma kutokana na kutofautiana kwa uzito kati ya mizani ya Bandari ya Dar es Salaam na Mizani ya Kibaha mkoani Pwani. 
  
Kutokana na mgomo huo hali ya usafiri katika barabara ya Morogoro ilikuwa tete na abiria kulazimika kutembea umbali mrefu. Abiria wengi walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

  
Wengine walishindwa kuendelea na safari na kulazimika kuvunja safari.
 Mwandishi wetu ameshuhudia mpaka saa 6: 00 usiku jana foleni ikiwa kubwa huku maofisa wa usalama barabarani wakijaribu kutatua tatizo hilo.
 
Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyanzo vya habari zimebainisha kwamba mgomo huo uliandaliwa kwa usiri mkubwa na kufanikiwa kwani maofisa wa  usalama hawakuwa na taarifa mpaka ilipofika majira ya saa 11:30 walipoanza kufuatilia na kubaini kuwapo kwa mgomo huo.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari