Takriban watu 50 wameuawa kwenye makabiliano kati ya polisi na wafasi wa Rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi.
Zaidi ya wanachama wengine miambili wa
vuguvugu la Muslim Brotherhood walikamatwa mjini Cairo,ambako vifo vingi
zaidi viliripotiwa.
Wafuasi wa Morsi waliandamana katika miji
kadhaa kote nchini Misri, huku jeshi likiadhimisha miaka 40 ya vita vya
mwaka 1973 katika ya waarabu na waisraeli.
Wafuasi wa Morsi wanasema kuwa aliondolewa mamlakani na jeshi mwezi Julai mwaka huu.(A.M)
Kipindi muhimu
Mamia ya watu walikusanyika katika medani ya Tahrir kuadhimisha siku hiyo.
Ndege za kijeshi zilionekana zikipaa angani huku jeshi likionyesha uwezo wake wa kulinda nchi.
Baadhi ya waliokuwa wamekusanyika mjini
humo walishangilia wakiwa wamebeba mabango yenye picha za mkuu wa ulinzi
Generali Abdel Fattah al-Sisi. Baadhi wanamtaka agombee urais katika
uchaguzi mkuu ujao.
Lakini mwandishi wa BBC Quentin
Sommerville mjini Cairo anasema kuwa wafuasi wa Morsi pia waliandamana
kwa wingi wakijaribu kuingia Tahrir kwa lazima huku wakimuita Generali
Sisi muuaji.
Askari wa usalama walitumia moshi wa
kutoza machozi na kufyatua risasi hewani kuwazuwia wafuasi wa Morsi
kufika medani ya Tahrir mjini Cairo.
Maelfu ya watu walishiriki Tahrir katika shughuli zilizotayarishwa na jeshi kuadhimisha siku hiyo.
Ghasia piya zilizotokea katika maandamano kama hayo kwenye miji kadha mengine ya Misri.