Like Us On Facebook

FAHAMU NYOTA YAKO LEO IJUMAA TAREHE 4-10-2013

                  MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Siku ya leo shughuli zako za kijamii zitakuwa za kufurahisha na zitakupa njia mpya ya kuweza kukutana na watu wapya au mambo mapya, usijaribu kujiingiza katika ubishani hasa na wapinzani wako, leo ni siku ambayo unatakiwa uwe mtulivu katika shughuli zako na utaona mafanikio.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ijumaa ya leo jaribu sana kuzidhibiti hisia zako na tumia hisia hizo kwa kukuletea mafanikio, leo ni siku ambayo utatambulika kwa kile utakachokifanya kwa jamii, usijaribu kulazimisha mambo unaweza ukapata matatizo.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Leo kuwa makini unaweza kupewa ahadi ambazo hazitekelezeki au za uongo hasa katika sehemu yako ya kazi au biashara, utapata bahati katika masuala ya fedha, fanya mambo na watoto wako na jiepushe na hali ambayo itakufanya uonekane hufai katika jamii hasa kwa wale wanaokupenda au kukuamini.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo panga mipango ya kutoka na familia yako kimatembezi, kitendo hicho kitakupa bahati na utajikuta ukipata mafanikio na maendeleo hasa katika mipango yako. Ni siku ambayo akiwa mkarimu utapata faida kubwa katika kila utakachofanya.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo usijaribu kufanya mambo ambayo unaona ni muhimu au kufanya mabadiliko katika mipango yako, kunaweza kukatoke mambo ambayo yasiyotabirika kwa upande wako na kuvuruga mipango yako, kuwa makini sana leo unaweza kupata matatizo madogo madogo au ajali ndogo ndogo.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo unahitaji kujipa changa moto au kujiuliza kuhusu mipango yako , utapata bahati lakini usiitumie bahati hiyo vibaya jaribu kuondoa migongano yoyote iliyopo au itakayotokea katika mipangilio yako ya siku ya leo na mambo yako yatafunguka.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Usipokuwa makini siku ya leo heshima yako inaweza kuvunjika, kuwa muangalifu kwa kila jambo utakalolifanya, safari kama unayo itakuwa nzuri, hata hivyo usiwe na khofu kuhusu biashara zako au mipango yako mambo yatafunguka na kuwa mazuri kwa msaada wa mtu mwingine .

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo jishughulishe sana na masuala ya watoto na shirikiana sana na wale ambao wanawasaidia watu, tumia muda wako kutimiza malengo yako na kutekeleza majukumu ambayo yalikuwa hayajatelezwa, utapata pesa iwapo utajituma zaidi siku ya leo.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Leo uanatakiwa uwe mbunifu, jishirikishe na vikundi au makundi ambayo yanaweza kukufanya upate kitu, leo tegemea kukutana na wageni kutoka mbali wageni hao watakuletea faida kubwa na mambo yatakuwa mazuri kama utajishughulisha na shughuli za kijamii.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Usimkopeshe mtu yoyote pesa siku ya leo unaweza ukapoteza au ukadhulumiwa, masuala ya kifedha leo uwe makini nayo sana unaweza ukapata hasara ambayo hukuitegemea.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Jaribu sana kuwa na tabia nzuri leo hasa nyumbani kwako, jaribu kumridhisha mpenzi wako na bahati yako itakuwa kubwa na manufaa utayaona

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Tabia yako ya kukasirika kupita kiasi itakuletea matatizo, kuwa makini katika kila jambo , mazungumzo yako, mipango yako, na shughuli zako uzifanye kwa umakini mkubwa vinginevyo utakwama.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari