Like Us On Facebook

VAN PERSIE AVUNJA REKODI YA MABAO YA KLUIVERT UHOLANZI AKIFUNGA HAT TRICK USIKU HUU

                MSHAMBULIAJI Robin van Persie amekuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Uholanzi kufutaia kufunga mabao matatu peke yake (hat trick) usiku huu katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Hungary.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United aliingia katika mchezo huo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, akiwa ana mabao 38 katika mechi 78 za Orange, na wenyeji hawakuwa na presha kwa kuwa walikwishajihakikishia tiketi ya Brazil Septemba mwakani.
Van Persie alifunga dakika ya 16 kabla ya Kevin Strootman na Jeremain Lens kuongeza.
Nahodha wa The Orange akafikia rekodi ya mabao 40 ya Patrick Kluivert karibu na mapumziko na akashangilia kwa kumkumbatia Kluivert, ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa Louis van Gaal katika timu hiyo.
Van Persie akavunja rekodi hiyo kwa bao la dakika ya 53 baada ya kazi nzuri ya Arjen Robben -- ambaye pia alimpa van Persie pasi ya bao la pili kabla ya kumpisha Dirk Kuyt dakika ya 61, Uholanzi wakiibuka na ushindi mnono wa mabao  8-1.
Mabao mengine ya Uholanzi yamefungwa na Strootman dakika ya 25, Jens dakika ya 38, Devecseri akajifunga dakika ya 65, Van der Vaart dakika ya 86 na Robben dakika ya 90, wakati la Hungary lilifungwa na Dzsudzsak kwa penalti dakika ya 47.
World class: Robin van Persie is now Holland's record goalscorer
Kiwango cha dunia: Robin van Persie sasa ni mfungaji bora wa kihistoria UholanziClinical: Van Persie is among the finest finishers in the world
Kitaalamu: Van Persie ni miongoni mwa wamaliziaji bora duniani
Explosive: Van Persie's finishes tend to be as accurate as they are powerful
Daka kama unaweza: Van Persie akifunga kwa ustadi wa hali ya juu
Aerial threat: Van Persie even scored with a header as Holland swept Hungary aside
Hata kwa vichwa: Van Persie akifunga kwa kichwa
Time to celebrate: Holland have already sealed qualification for the World Cup
Wakati wa kushangilia: Wachezaji wa Uholanzi wakishangilia ushindi wao wa 8-1
Goalscorer: Jeremain Lens scored Holland's third goal
Hata huyu mbaya: Jeremain Lens akiifungia Uholanzi bao la tatu
Attacking flair: The Dutch were rampant against Hungary
Wachezaji wa Uholanzi wakipongezanaProlific: Patrick Kluivert previously held Holland's goalscoring record
Ameondolewa kileleni: Patrick Kluivert ndiye alikuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Uholanzi

Katika mchezo mwingine, bao pekee la Andriy Yarmolenko dakika ya 64 limeipa Ukraine ushindi wa 1-0 dhidi ya Poland na kufufua matumaini ya kucheza Kombe la Dunia.
Match winner: Andriy Yarmolenko celebrates after scoring the only goal of the game against Poland
Mshindi wa mechi: Andriy Yarmolenko akishangilia bao pekee dhidi ya Poland

Nayo Ubelgiji imejikatia tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002 baada ya mshambuliaji anayecheza kwa mkopo Everton kutoka Chelsea, Romelu Lukaku kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Croatia.
Matokeo hayo yanamaanisha vinara hao wa Kundi A, Ubelgiji hawawezi kukamatwa kwa pointi zao 25 walizovuna kwenye mechi tisa wakiwa wamebakiza mechi moja nyumbani na Wales Jumanne.
Goal hero: Romelu Lukaku's double strike saw Belgium qualify for next summer's World Cup in 2014
Shujaa: Mabao mawili ya Romelu Lukaku yameipeleka Ubelgiji Fainali za Kombe la Dunia mwakani
Goal hero: Romelu Lukaku's double strike saw Belgium qualify for next summer's World Cup in 2014

Kiungo wa zamani wa Liverpool, Alberto Aquilani alifunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi Italia ikitoa sare ya 2-2 na Denmark katika mchezo wa Kundi B.
Mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner alifunga mabao mawili na kuwafanya waongoze 2-1, lakini ambayo tayari imekwishafuzu ilipata mabao yake kupitia kwa Daniel Osvaldo  na Aquilanina kuiongezea ugumu Denmark wa kwenda Brazil.
All square: Nicklas Bendtner beats Italy keeper Gianluigi Buffon to make it 1-1
Kitu hicho: Nicklas Bendtner akimtungua kipa wa Italia, Gianluigi Buffon na kufanya 1-1Back in it: Bendtner celebrates his first strike with Liverpool defender Daniel Agger
Shangwe: Bendtner akishangilia bao lake la kwanza na beki wa Liverpool, Daniel Agger
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari