Like Us On Facebook

AFYA:MAUMIVU YA KORODANI (TESTICULAR PAINS)

KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha maji kinachozunguka korodaniili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo kubwa. Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na matatizo mbalimbali tuliyoelezea katika toleo lililopita.

Mwanaume mwenye korodani moja anaweza kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa, kitu cha msingi akapimwe hospitali kuona
uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye hana korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo
wa kumpa mimba mwanamke. Tatizo la kuwa na korodani moja au kukosa kabisa tutakuja kuliona katika makala zijazo.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Maumivu ya korodani hutokea katika korodani au haswa moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kuwa makali na ya muda mfupi,yanakuwa makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena yakiwa makali sana kama mwanzo au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayokunyima raha. Maumivu ya korodani yanaweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier’s gangrene’ au inatamkwa ‘Fonias gangrini’.

Vilevile inaweza kutokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa ‘Testicular Torsion’. Matatizo haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona katika makala zijazo.

CHANZO CHA TATIZO
Maumivu ya korodani yana vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takriban zaidi ya miezi mitatu. Maumivu makali na ya ghafla
huwa hayavumiliki na huwa na tiba ya dharura. Maumivu haya sugu huwa kwa kipindi fulani hasa kwa wanaume ambao wametoka kufunga uzazi ‘Vesectomy’ lakini baadaye hupoa. Vilevile husababishwa na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha ugumba.

Tutakuja kuona katika matoleo yajayo. Vilevile korodani inaweza kuwa na vivimbe kwa ndani,pembeni au juu ya kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi vinaweza kuwa na mishipa ya damu iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo kawaida, mbegu za kiume kujikusanya na kushindwa kutoka na mengine ya kitaalam ambayo pia tutakuja kuyaona.

Yote haya humsababishia mwanaume ugumba. Maumivu pia husababishwa na kuumia korodani au baada ya kufanyiwa upasuaji kama tulivyokwishaona hapo awali. Maumivu yatokanayo na korodani au kende kujinyonga huwa makali sana na korodani zikiguswa
huuma sana na kawaida huendelea hivyo kwa masaa yasiyozidi sita.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0713354389, 0752133700 kwa maelezo zaidi.


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari