Katika kesi
hiyo, walalamikaji wanaiomba mahakama hiyo itangaze kuwa, sheria iliyopitishwa
na Bunge inayotaka kila mtumiaji wa simu ya mkononi kukatwa sh. 1,000 kila
mwezi kwa kila laini ni kandamizi.
Taasisi hiyo
ilidai kuwa, watumiaji wengi wa simu za mkononi hawana uwezo wa kukatwa fedha
hiyo kwa mwezi na kusisitiza itawaathiri watumiaji wa huduma hiyo.
Kwa mujibu wa
madai ya walalamikaji, sheria hiyo inakiuka matakwa ya katiba ya nchi ya uhuru
wa kupashana habari na kuiomba mahakama kuifuta sheria hiyo wakidai ni
kandamizi.
Mawakili wa
walalamikaji kutoka Kampuni ya uwakili ya Rex, Lugano Mwandamo na Merkizedeki
Lutema, walidai wateja wao wanataka mahakama imzuie Waziri wa Fedha kupitia
Mamlaka ya Mapato (TRA), kutotoza kodi hiyo hadi maombi yao yatakapotolewa uamuzi.Katika kesi
hiyo, upande wa serikali uliwakilishwa na wakili Kelley Mwitasi.
-Majira