Like Us On Facebook

ZIJUE DALILI 8 ZA MWANAMKE ANAYETOKA NJE YA NDOA.


Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini
kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake,
inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo
kwa mwanaume.

Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na
nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke
huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume.

Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza
kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo
kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:



1. KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga
kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea
kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu
hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni
huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani.
Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

2. KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu,
hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata
nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila
sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.

Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya,
lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana
kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti
unaofanywa.
anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi
atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi.

Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo
wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo
angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba
kwa siri.

4. KUANZISHA VURUGU:Kuna wakati mwanamke
anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate
nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda.
Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na
vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa
hawara yake.

5. KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka nje ya
ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe,
yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo
wanandoa huwa wanashiriki.

Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri,
kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.

6. KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa
nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya
ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au
ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana.
Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu
nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara
kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa
na uhusiano nje ya ndoa yake.

7. KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka
nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake.
Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana
kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu ambacho
tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi
wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke
anayetoka nje , hasa katika hatua zake za awali za
kutoka nje.

8. KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati mwanamke
anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana.
Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke
anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane tu”
hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke
anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari