MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu kama
Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi anayejulikana
kwa jina moja la Nagar.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana huyo
aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu na
Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu
sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba
ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo
hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika
sehemu mbalimbali za starehe.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini baada ya
kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo, alipiga
simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema
anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema
kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.