
MSANII wa kike wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kwa kusema kuwa mwanaume sahihi kwake na anayestahili kumuoa ni Rashid Mizengwe ‘Kingwendu’ kwa kusema anaamini ndiye anaweza kuwa mwaminifu na kuishi naye kwa raha tofauti na mwanaume mwingine yoyote endapo atapata bahati ya kuolewa naye.
Rayuu alisema hayo alipoongea na Maskani Bongo katika mahojiano yake na gazeti hili kuhusu mume gani bora kwake na angependa kuolewa naye na kuishi kama mke na mume, msanii alisema kuwa anahitaji mtu aliyetulia sambamba na umri wa makamo na mtu anayempenda sana kama awe mumewe ni msanii mwenzake Kingwendu au