Mtu mmoja aliefahamika kwa Jina la Nice Mtega fundi mkuu wa Meli ndogo ya mizigo iitwayo MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro anahofiwa kufa maji baada ya kutoweka toka kuzama kwa meli hiyo katika bandari ya Kilwa masoko.
Akiongea
na mwandishi wetu, meneja wa Bandari ya
Kilwa, Bw. Iddi Omary, alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana
jioni ikitokea songosongo na kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za
maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo Nahodha wa Meli
hiyo Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka
ila Nice Mtega aliekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa.
Juhudi za
kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado
hazijajulikana