Katika baadhi ya sehemu duniani watu
wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao
mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini
ya kiwango,
hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu,
vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.
Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana
na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata
hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo
yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo
yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo
hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.
Madhara ya
kujichubua ni yapi?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata
kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka
kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro,
kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu
pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika
krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya
kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara
moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.