MWANADADA anayetamba na kibao cha Mimi na Wewe, Mwanaisha Said Nyange
‘Dayna’ amefunguka kuwa hataki kabisa kumzungumzia msanii mwenzake,
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mwanaisha Said Nyange ‘Dayna’.
Dayna aliyasema hayo hivi karibuni alipoulizwa kuhusiana na bifu lake
na Diamond lililotokana na kumwibia wimbo wake ambapo alisema hataki
kumzungumzia kabisa Diamond kwa sababu hataki malumbano kwani hivi
karibuni amezungumza maneno mbofumbofu kwenye vyombo vya habari.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Mimi sitaki malumbano na Diamond kwa sababu amekuwa akizungumza
mengi sana kwenye vyombo vya habari mengine ya kuniponda na mengine ya
kawaida hivyo sitaki malumbano kabisa mimi niko kikazi zaidi yeye
aendelee tu”, alisema Dayna.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.