"Nilishtuka sana na kushindwa kuondoka eneo hilo mpaka wafanyakazi wenzangu walipoondoa mashine na kutoa mkono wangu kisha kunipeleka hospitali" Alisema Xiao, akielezea ajali hiyo iliyotokea mwezi uliopita.
Baada ya kupelekwa katika hospitali mahiri nchini China, saa saba baada ya ajali hiyo, madaktari walisema wataurudisha mkono huo ila siyo moja kwa moja.
Ili kuzuia mkono wa Xiao usiharibike, madaktari waliamua kuuunganisha katika kifundo cha mguu ambapo ulikaa kwa mwezi mzima baada ya kupona majeraha mengine ndipo walipourudisha katika eneo lake. Madaktari wanadai Xiao atapona vizuri na mkono wake utafanya kazi kama zamani.
-Metro