Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa mahakamani leo.
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro leo imetupilia mbali ombi la
kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda. Ponda anakabiliwa
na mashitaka matatu; ambayo ni kutokutii amri halali, kuharibu imani za
dini na kushawishi kutenda kosa. Ombi la kufutiwa shitaka moja
liliwakilishwa na Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro, mahakamani hapo
Septemba 17, mwaka huu, akitaka shitaka la kwanza la kutotii amri halali
linalomkabili mteja wake lifutwe. Wakili Nassoro alidai kuwa mahakama
hiyo haina uwezo kisheria kusikiliza shitaka hilo, vinginevyo
lifunguliwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kesi hiyo
imeahiriswa mpaka Novemba 7 mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza
mashahidi wa kesi hiyo. Sheikh Ponda amerudiswa rumande-GPL