Like Us On Facebook

NYUMBA ZA MCHEZAJI MRISHO NGASA ZANUSURIKA KUCHOMWA MOTO

 
Mchezaji wa Yanga Mrisho Ngasa alikuwa amesema kuwa asipofunga goli ama kutoa pasi itakayo zaa goli zidi ya simba mechi ya jana basi angechoma moto nyumba zake tano .....Lakini simesalimika baada ya  kuwa mfungaji wa goli kati ya magoli matatu waliyo pata yanga .......Mechi hiyo simba na yanga walitoka droo ya 3-3
CHEKI MIJENGO YAKE ILIYONUSURIKA
Hakuna maslahi makubwa aliyopata Bukoba, zaidi alikuwa anatafuta njia ya kutokea katika soka ya Tanzania na tangu Yanga SC hadi sasa unaweza  kusema Mrisho ametumia kipindi hicho kuchanga  vyema karata zake. Anamiliki nyumba tano, tatu  zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam- na ana gari  nane, wakati huo huo akaunti yake wakati wote ikiwa ‘imefulia sana’ ina Sh. Milioni 20. Akiwa bado anategemea soka kama ajira yake, Ngassa amekwishaanza kujipanga kwa maisha ya baada ya soka na katika mahojiano  wiki hii anasema anafanya biashara ya usafirishaji na kilimo.
    SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahia  maisha ya mpira. Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wa
 kizazi chake, kwamba amewaacha mbali. Amecheza klabu nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012 na sasa amerejea Jangwani,
 

                                         Ngassa akia na bibi na babu
                                          Ngassa katika kaburi la shangazi yake                                                        Ngassa na watoto wake

“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya
shughuli za nyumbani wakati wote na mbili nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”. Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanua zaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwa mwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.    “Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa sitegemei kurudi shule kusomea chochote, nitafanya biashara. Nimekwishaanza kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”. “Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za >kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na siku moja nitatatambulika kama mwanasoka wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, tayari nina mashamba kama matatu, hapo nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni  biashara kubwa,”anasema Ngassa. 
Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.  
Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu
Nyumba nyingine ya Mwanza


Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili,  ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana
 na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora,ili wakue vizuri. Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Stars katika mechi za kuwania kucheza Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),Ngassa ameenda likizo Mwanza tangu Jumatatu na anatarajiwa kuripoti kazini, Yanga SC Jumapili. Ngassa alijaribu sana kuibeba Stars akitoa krosi ya bao lililofungwa na Amri Kiemba na kukaribia kufunga mara mbili, lakini Tanzania ikalala 3-1 mbele ya Uganda mjini Kampala na
kutolewa CHAN.  Amekubali matokeo na kwenda kusalimu wazazi, ndugu, jamaa na marafiki baada ya mwaka mzima wa kuwa kazini Dar es Salaam. Akiwa huko, Ngassa alitembelea bibi na babu zake, ndugu, jamaa na marafiki hadi vijijini na pia kuzuru kaburi la shangazi yake aliyefariki mwezi mmoj uliopita yeye akiwa ametingwa na majukumu ya kitaifa. Gari la Ngassa la MwanzaGari lingine la Ngassa

Ngassa aliwatemebelea watoto na kuwazawadia mipira ili wacheze soka, akiwahamasisha kujibidiisha na wao watakuwa  kama yeye siku moja, kwani hata yeye aliaanzia kama wao.  Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mno kutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana  mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake. Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada ya sadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoska nyota Tanzania.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari