Mamlaka nchini Nigeria zimesema kuwa hakukuwa na ulinzi katika chuo cha Kilimo ambako wanafunzi 50 waliuawa kwa kupigwa risasi wakiwa wamelala.
Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya tukio hilo lililotekelezwa na wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wenye itikadi kali ya Kiislam wa kundi la Boko Haram katika chuo hicho katika jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Ofisa mmoja wa serikali amesema, serikali na jeshi la wataimarisha ulinzi kwenye maeneo ya shule na kuongeza kuwa licha ya shambulio hilo masomo yataendelea kama kawaida.