Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, aliyehamia Arsenal kwa Pauni Milioni 42.5 katika siku ya mwisho ya usajili, aliambiwa na Real Madrid kuweka kazi yake ya soka mbele baada ya kuonekana kuelemewa na penzi la aliyekuwa Miss Venezuela, Aida Yespica, kwa mujibu wa gazeti la El Mundo la Hispania.
Mkwanja mnene: Ozil ametua Arsenal kwa Pauni Milioni 42.5
Amemshika: Ozil anafikiriwa kutekwa kimapenzi na aliyekuwa Miss Venezuela, Aida Yespica ambaye amekuwa akimfuata poppote Ulaya anapokwenda kucheza
Ozil ameripotiwa kusafiri hadi Italia kila anapopata mwanya kidogo ili kupata fursa ya kuwa na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 31 mjini Milan au katika hoteli yake mjini Paris.
Anakadiriwa kutumia kiasi cha Pauni 15,000 kila wiki mbili kwa ndege binafsi, inayompeleka kwa Yespica.
El Mundo limeripoti kwamba safari za asubuhi na mapema zimezidi na kiasi cha kufikia kushusha kiwango chake cha soka.
Utata: Baadhi ya mashabiki wa Madrid wamekasirika juu ya kuuzwa kwa Ozil
Mpenzi wake mpya, Many Capristo anafikiriwa kutaka kumfuata Uingereza ili kuwa karibu naye, lakini gazeti la The Sun le leo limeripoti kwamba amekaa ushauri wa kutafuta nyumba karibu na viwanja vya mazoezi vya Hertfordshire.
Capristo anayetarajiwa kuwa nyota mpya katika wake na wapenzi wa wachezaji, maarufu kama WAGs - mahusiano yake na mwanasoka huyo yamepewa jina Posh na Becks wa Ujerumani.
Ozil, mwenye asili ya Uturuki, ni Muislamu, lakini mpenzi wake amekuwa maarufu Ujerumani kwa sababu ya muziki na kudansi katika show ya Televisheni
Penzi la nguvu: Mesut Özil na mpenzi wake mwimbaji, Mandy Capristo wanatarajiwa kuhamia London baada ya mchezaji huyo kujiunga na Arsenal akitokea Real Madrid kwa Pauni Milioni 42.5
Pamoja: Wawili hao wamekuwa kwenye wimbi la mahaba kwa zaidi ya mwaka.
-BIN ZUBEIRY
-BIN ZUBEIRY