Watau hatari; Kutoka kulia ulimwengu, Mputu na Samatta jana |
Mazembe ikazinduka na kupata bao la pili dakika ya 16 lililofungwa na Tessor Mputu, ambaye aliipangua safu ya ulinzi ya Setif na kumtungua kipa Sofiane Khedairia.
Ulimwengu akaifungia Mazembe la tatu dakika ya 27, akimalizia krosi maridadi ya Mbwana Samatta, ambaye alimtoka Abdelghani Demmou.
Jinsi Mbwana Samatta anavyopendwa Mazembe |
Samatta akimiliki mpira mbele ya beki wa Setif |
Ulimwengu akitafuta njia ya kuchomokea |
Tressor Mputu akitafuta mbinu za kumtoka mtu |
Mazembe ilipewa penalti dakika za majeruhi, lakini kiungo Ngasanya Ilongo akapaisha.
Samatta akipambana katika mchezo wa jana |
Samatta akivizia mpira udondoke afanye mambo |
Stopila Sunzu anakaba |
Robert Kidiaba akiwa amedaka |
FUS Rabat, ambayo itamaliza na Mazembe katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo B, inaweza kuungana na akina Samatta na Ulimwengu ikiwa itawafunga wenyeji CA Bizertin ugenini Tunisia leo. Bizertin na FUS zimefungana kwa pointi tano kikla moja.