WAKALA wa staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes amedai kwamba mchezaji wake ni staa aliyekamilika zaidi kuliko nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Ronaldo, 28, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano ambao unamfanya awe mwanasoka anayelipwa zaidi duniani huku Mendes akiamini kuwa staa huyo anastahili kwa sababu amekamilika kuliko Messi licha ya ukweli kwamba Barcelona ndiyo timu bora zaidi ulimwenguni kwa sasa.
“Cristiano Ronaldo ni mchezaji aliyekamilika zaidi kuliko Messi. Licha ya heshima kubwa niliyonayo kwa Neymar, lakini hakuna ubishi kwamba hakaribii uzuri wa Ronaldo,” alisema wakala huyo ambaye pia anawasimamia Jose Mourinho na Radmel Falcao pamoja na kundi kubwa la wachezaji wa Kireno na Kibrazili