PICHA ya mbele ya kikosi cha Manchester United imebadilika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27 huku David Moyes akitokea katikati mbele yangu Sir Alex Ferguson astaafu.
Picha mpya imetolewa kwenye ukurasa wa Twitter klabu, na Moyes akiwa amepo katikati ya Nahodha wake, Nemanja Vidic na kiungo mkongwe, Ryan Giggs.
Picha hiyo pia inamhusisha mchezaji mpya, Marouane Fellaini, ambaye amepozi katikati kwa mstari wa mwsiho kabisa, na Wayne Rooney, ambaye alivumishwa kutaka kuondoka klabu hiyo majira ya joto, amepozi mbele kulia. Taji la Ligi Kuu ya England na Ngao ya Jamii pia yamo pichani.
Kikosi kipya: Manchester United imetoa picha mpya kwa ili ya msimu mpya na David Moyes, Marouane Fellaini na Wilfried Zaha ni miongoni mwa waliomo
KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED 2013-2014
Kikosi cha Manchester United(Nyuma kabisa kutoka kushoto:) Danny Welbeck, Phil Jones, Chris Smalling, Jonny Evans, Marouane Fellaini, Rio Ferdinand, Michael Carrick, Robin van Persie
(Katikati kutoka kushoro:) Ofisa Garry Armer, Mchambuzi wa viwango vya mchezo, Paul Brand, Mkuu wa Ufiti, Tony Strudwick, Antonio Valencia, Darren Fletcher, Wilfried Zaha, Adnan Januzaj, Fabio da Silva, Ofisa Rod Thornley, Mtunza Vifaa, Alec Wylie, Physio Neil Hough
(Mstari wa pili kutoka kushoto:) Mtunza vifaa Msaidizi, Ian Buckingham, Daktari Rob Swire, Dk Steve McNally, Alexander Buttner, Sam Johnstone, Anders Lindegaard, David de Gea, Ben Amos, Ashley Young, kocha Phil Neville, Ofisa Andy Caveney, kocha wa makipa, Chris Woods.
(Mbele kutoka kushoto:) Shinji Kagawa, Rafael da Silva, Anderson, Nani, Assistant Manager Steve Round, Ryan Giggs, Kocha David Moyes, Nemanja Vidic, Kocha Jimmy Lumsden, Patrice Evra, Javier "Chicharito" Hernandez, Tom Cleverley na Wayne Rooney
Mataji matatu: Sir Alex Ferguson, Roy Keane na wakiwa na mataji matatu ambayo klabu ilishinda msimu wa 1999-2000
Mabingwa wa Ulaya: Matt Busby, Bobby Charlton na George Best katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ulaya kwa kuifunga Benfica mwaka 1968
Mitambo ya umeme: Ron Atkinson na kikosi cha msimu wa 1982-1983 wakiwa na bidhaa za wadhamini wa wakati huo, Sharp
Wanatembea: Wachezaji wa Manchester United wakiondoka Uwanja wa Old Trafford baada ya kupiga picha ya timu
Anakosekana: Sir Alex Ferguson hayumo kwenye picha mpya baada ya kustaafu