Akizungumza na ITV wakati wa utambulisho wa mtambo huo uliofanyika hospitalini hapo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji Dk.Marina Njelekela amesema mtambo huo utaanza kufanya kazi rasmi mapema mwezi ujao na kubaini kuwa serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa wagonjwa waliokuwa wanaenda kutibiwa nje na nchi na kutoa wito kwa kampuni zote za bima ya afya nchini kuwalipia wateja wao wanaohitaji huduma mbalimbali za moyo kutokana na gharama zake kuwa juu.
Naye mkuu wa idara ya magonjwa ya upasuaji wa moyo na utabibu hospitali ya muhimbili Dkt.Robert Mvungi amesema pamoja na upatikanaji wa mtambo huo bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalamu ambapo amebaini kuwepo kwa madaktari 121 tu kati ya 365 wanaohitajika.