Like Us On Facebook

FRANCIS CHEKA AAMUA KURUDI SHULE..!! ANAANZA PRE FORM ONE WIKI IJAYO


 

Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ambaye hivi karibuni alipewa zawadi ya  kiwanja na Rais Jakaya Kikwete baada ya ushindi wake dhidi ya bondia wa Marekani, ameamua kurudi shule.Cheka anasema hakupata nafasi ya kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba. “Mimi sikusoma niliishia darasa la saba, lakini nimeamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph”.
“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine 
-mwananchi
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari