Like Us On Facebook

"BASATA KUNA KITU WANATAFUTA KUTOKA KWANGU....." NEY WA MITEGO

Siku chache zilizopita mwana Hip Hop kutoka pande za Manzese Nay Wa Mitego alipokea barua kutoka BASATA inayomtaka kubadili aina ya mavazi anayovaa katika show zake (mlegezo/mtepesho) ambayo hayaendani na Tamaduni za kitanzania.

kizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea.


“Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay.


Aidha  katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya kufanya kwaajili ya kuboresha  maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.



“Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi  sana za kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay, hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini  maybe wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari