Like Us On Facebook

MOHOMBI,DAVIDO,NAY WA MITEGO NA DIAMOND KUPIGA SHOW YA BURE LEO KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB KUANZIA SAA TISA ALASIRI

Kutokana na kutokea hitilafu ya umeme Alfajiri ya leo kwenye show ya Serengeti Fiesta Dar, iliyopelekea baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajia kupanda jukwaani kutumbuiza akiwemo Davido, Mohombi, Diamond, Nay wa Mitego na wengine kushindwa kupanda, leo kuanzia saa tisa, wasanii hao watapanda tena jukwaani kuzikonga nyoyo za mashabiki wao bila kiingilio chochote.
 
Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12.Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari