Ingawa anaandamwa na watu hao msanii huyo hakuwa tayari kuwataja wala kuwaweka wazi watu hao anaodai kumtishia maisha.
Msanii huyo anatamba na single yake inayojulikana kwa jina la 'Salaam Zao' ameandika taarifa hiyo ya kuandamwa na watu hao ambao hadi sasa hawajajulikana ni akina nani katika ukurasa wake wa Istagram.
Ney aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya watu wanamchukia yeye kutokana na kazi zake za muziki huku akibainisha kuwa watu hao wanatamani yeye apoteze maisha.
"Huu muziki sasa utanitoa roho sina ugomvi na mtu lakini kumbe kuna watu wananichukia kweli na wanatamani hata nife leo au wanitoe roho, mimi nafanya muziki vita yenu juu yangu namuachia mungu" aliandika katika mtandao wake wa Istagram.
Aliweka wazi kuwa yeye anaamini anafanya kazi nzuri hivyo hakuna mtu yoyote wa kumshusha wa kumrudisha nyuma, huku akisisitiza kuwa hata wakitumia imani za kishirikina hawatafanikiwa kwani yeye si wa kawaida.