Ni video ya wimbo ambao wametumia melody na beat ya single ya P Square ‘Personally’ na kuiweka October 26 2013, watu wengi waliyoiona hasa ukitazama mitandao ya kijamii kama facebook na twitter, maoni mengi yameiponda hii video na wimbo wenyewe ambao waamini umevuka maadili ya Kiafrika na kisanii pia wamevuka mipaka.
Sehemu ya waliotoa maoni wanalalamikia udhalilishwaji wa Wanawake na
wengine wanalalamikia sehemu ya mashairi pamoja na vingine
vinavyoonekana kwenye video.