Picha ya utupu iliyosambaa ya Mwigizaji Koletha Raymond ‘Koletha’.
Koletha aliyasema hayo ikiwa ni siku chache tu baada ya mitandao
kadhaa kusambaza picha ya utupu inayoonesha sehemu ya kiuno, ikidaiwa
kuwa ni ya msanii huyo ambapo paparazi wetu alipomhoji kuhusiana na
picha hiyo, alitiririka:“Hiyo picha siyo yangu. Mimi siwezi hata siku moja kusaka usupastaa kwa kupiga picha za uchi, kwanza sipendi na sitaki kufanya hivyo sababu ninajiheshimu tofauti na wenzangu wanaoendekeza mambo hayo wakati hawana kazi hata moja sokoni,” alisema Koletha.