KLABU
ya Manchester United lazima iamue kumpeleka Danny Welbeck kufanyiwa
upasuaji wa goti ambao utamuweka nje mshambuliaji huyo wa England kwa
wiki nyingine tano.
United tayari inamkosa kiungo Michael Carrick, ambaye atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi.

Majeruhi: Danny Welbeck atalazimika kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamuweka nje kwa wiki nyingine tano

Pigo United: Michael Carrick atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi
Matatizo yanayomsumbua Welbeck tayari yamemfanya amekosa mechi sita zilizopita za United.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 22 anapatiwa matibabu yanayompa matumaini
anaweza kuepuika upasuaji, lakini United inahofia italazimika kumpeleka
kwenye upasuaji ikiwa hali yake haitaimarika.
Welbeck amekwishafanyiwa upasuaji wa goti mara mbili. Marouane Fellaini pia anaweza kuwa nje kwa wiki hadi 10 atakapofayiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia.

Carrick alikwenda kwenye ziara ya mashindano ya dunia ya DP Dubai


Carrick aliungana na Caroline Wozniacki kumtazama Rory McIlroy akicheza

David Moyes atawakosa Carrick na Welbeck katika mechi na Spurs na Everton