Katika hali isiyo ya kawaida, askari mmoja wa jeshi la Polisi amepokea kichapo toka kwa kundi la
wafugaji na kuporwa silaha aliyo kuwa nayo {bunduki} aina ya SMG.
Askari huyo amekutwa na janga hilo wakati wa doria ya kuondoa waharibifu wa bonde la kilombero. Wafugaji walimshambulia kwa fimbo kichwani kisha kumpora silaha na kutoweka nayo.
Jeshi la polisi limefanikiwa kumnasa mshukiwa mmoja ambaye anaisaidia polisi.