Wastara Juma.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wastara alisema kuwa anajisikia
furaha kupewa ofa hiyo kutoka kwa wadau wa tasnia ya filamu pande za
Kenya ambao wamekuwa wakivutiwa na kazi zake.“Nimepewa ofa ya mguu bandia wa bure ambao utanisaidia, pia nitafanyiwa uchunguzi wa mwili mzima pamoja na mambo mengine. Nina furaha kwa heshima hiyo niliyopewa na wadau hao na kwa msaada wao huo, Mungu atawalipa,” alisema Wastara.
Enzi za uchumba wake na marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ walipata ajali iliyosababisha Wastara kukatwa mguu ambapo aliwekewa wa bandia. hivyo mguu huo aliopewa ni wa pili ili kama atahitaji abalishe ule wa zamani.
-GPLA