MWIGIZAJI wa sinema zao la Shindano la Kimwana Manywele, Husna Idd ‘Sajent’ amesema haumizwi kichwa na ndoa ya mzazi mwenzake, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na mwanadada Janeth Sospeter.
Akiongea na GPL jijini Dar es Salaam Sajent alisema kitendo cha mzazi mwenzake huyo kufunga pingu za maisha hivi karibuni hakimsumbui kabisa akili kwani anaamini hata yeye anaweza kumpata mtu na kufunga naye pingu za maisha muda si mrefu.
“Hilo la kufunga ndoa mimi wala halinitishi kwa vile matunzo ya mtoto ananipatia sina presha na ndoa yao, acha waishi kwa raha zao nami nakula bata kivyangu,” alisema Sajent.