Like Us On Facebook

MAMA MMOJA AMESEMA "NITAMNYONYESHA MWANANGU HATA KWA MIAKA 10 KAMA AKITAKA..."


 
 Maha Al Musa akimnyonyesha mwanaye mwenye umri wa miaka mitano. MWANAMKE mmoja wa New South Wales, nchini Australia, aitwaye Maha Al Musa, amekuwa akimnyonyesha mwanaye ambaye sasa ana umri wa miaka mitano.
 
 Maha Al Musa akipozi na wanaye watatu.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 51 ambaye ni msanii wa burudani ya unenguaji, aliacha kuwanyonyesha watoto wake wawili hadi walipofikia miaka miwili kila mmoja, lakini mwanaye wa sasa ambaye ni wa tatu, ameamua kuendelea kumnyonyesha kwa vile alihisi alikuwa ‘amebarikiwa’ na ameahidi kwamba ataendelea kumnyonyesha hadi afikie umri wa miaka kumi iwapo atataka kuendelea kunyonya.
Maha aliwaachisha watoto wake wawili -- Kailash ambaye sasa ana miaka 16, na  Tariq, (13), wakiwa na miaka miwili kila mmoja.
 
Jarida la Time lililomwonyesha Jamie Lynne Grumet akimnyonyesha mwanaye mwaka jana.
Al Musa amefuata nyayo za Jamie Lynne Grumet (26) wa Los Angeles, Marekani,  ambaye aliwashangaza watu baada ya kutolewa na jarida la Time lililomwonyesha akimnyonyesha mtoto wake wa miaka minne.
Wakati mtoto wake Al Musa amefikisha miaka mitano, mama huyo anasema hajali wanachosema watu kuhusu jambo hilo
“Ninaamini kuendelea kwake kunyonya kunamjengea kinga dhidi ya magonjwa  kwani yuko katika afya njema na utulivu kuliko watoto wengine,” anasema mama huyo.
Naye Grumet ambaye alinyonyeshwa na mama yake hadi kufikia umri wa miaka sita na  aliyekuwa akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni, aliunga mkono unyonyeshaji wa namna hiyo, japokua watu hushangaa.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari