Like Us On Facebook

UGUMU WA AJIRA:APARAMIA MAGARI YA WATU NA KUANZA KUYAOSHA BILA KUAMBIWA

                  Kijana huyu amekuwa kero kwa wakazi wa Dar es Salaam hususani waendesha magari kwa tabia yake ya kuyaparamia na kuanza kusafisha vioo pasipo ruhusu ya wamiliki. Kijana huyu huzunguka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam na mara panapokuwa na foleni huvua shati lake chafuchafu na kuparamia vioo kisha kuanza kuvifuta. Hapa alinaswa na kamera yetu katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la Bamaga akipangusa vioo vya magari kwa shati lake pasipo kuambiwa kufanya hivyo. Mara amalizapo kazi hiyo hudai malipo kwa wenye gari ambao baadhi yao hulipa wakati wengine wakimsusia.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari