Like Us On Facebook

HOFU YATANDA MSANII RAY KUSOMEWA ALALBADIR KUVIMBISHWA “BUSHA” KISA MKE WA MTU, ATAKIWA KUMUOMBA RADHI RAFIKI YAKE FRANK MTAO KUHUSU MKEWE, CHUCHU HANS APIGWA TARAKA!

                   Frank Mtao ambae amedaiwa kumpa taraka mkewe Chuchu Hans kisa  rafiki yake Ray






 Moja ya Layout ya gazeti pendwa liliripoti habari ya fumanizi la Ray na Chuchu Hans.

                                           Chuchu Hans akiwa na mtoto wake

Ni kipindi kirefu sasa kumekuwa na madai ya kashfa ya msanii Vicent Kigosi “Ray “ kudaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi  na mke wa mtu ambae pia ni msanii wa bongo muvi Chuchu Hans huku vyombo mbalimbali vya habari hasa magazeti pendwa yakiripoti kwa kina tukio hilo.

Habari za ziada zilizonaswa  toka kwa mtu wa karibu na familia ya Frank Mtao zilisema kuwa taarifa za Ray kutembea na Chuchu Hans zinaukweli kubwa sana kwani hata tukio la hivi karibuni la Ray kufumaniwa na akiwa na Chuchu Hans wanazichukulia kama ni za ukweli kwani Johari ambae ndiye mchumba harisi wa Ray aliwahi kukutana na mmoja wa wanafamilia wa Frank Mtao na kuwaeleza kila kitu.

Hata hivyo  Ray kwa inadaiwa kusababisha ndoa ya Frank Mtao kuvunjika kwani hivi karibuni Frank Mtao ambae anaishi nchini Austaralia baada ya tukio la kufumaniwa mkewe na Johari akiwa na Ray nyumbani kwa Chuchu mtangazaji huyo amemtwanga taraka Chuchu Hansa ambae sasa hivi maisha yanamwendea kombo baada ya kushindwa kulipia pango ya nyumba maeneo ya Msasani na kuhamia Mwananyamala kwa Mama Zacharia uswahili.

Aidha  katika hali isiyokuwa ya kawaida Ray amekuwa akimng’ong’a Frank Mtao kwa kujifanya kuwa ni rafiki yake wa karibu  na mara nyingi amekuwa akimpigia simu Frank Mtao na kumuweka roud speak wakati akiwa na Chuchu Hans.

Chanzo hicho kiliendelea kueleza “ Kwa kweli inasikitisha kuna siku Ray alikuwa na Chuchu Hans alimpigia simu Frank Mtao na kuanza kutaniana nae na baadae alimuuliza kama huko hana demu hali na Frank alimjibu kuwa anae wa kuzugia na Ray alihitaji Frank amtumie picha yake na Frank alifanya hivyo na picha hiyo aliiona Chuchu Hansa na baadae palizuka mtiti mzito” Alisema dada huyo ambae alisema yeye ni binamu wa familia ya Frank.

Aidha watu mbalimbali wameonesha wasiwasi wao kuwa huenda Frank Mtao akalipa vibaya kwa kumsomea alalbadir msanii Ray na kama kweli tuhuma anazotuhumiwa zitakuwa za kweli msanii huyo atakuwa amejipatia matatizo makubwa kutokana na dua hiyo jinsi inavyofanya kazi kama tukio lina ukweli na huenda akashushwa “busha” na baadae kulazimika kutembea na mkwangwaju.
-XDEEJAYZ

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari