Like Us On Facebook

CHICHARITO ATAJA SABABU KWA NINI ATAONDOKA MAN UNITED

              MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amesema anaweza kuondoka Manchester United ili kusaka timu ambayo atapata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
Mshambuliaji huyo anayefahamika kama Chicharito hapewi nafasi kubwa katika klabu ingawa mwezi uliopita aliifungia timu hiyo bao la ushindi katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One dhidi ya Liverpool na zaidi ya mechi hiyo alianza katika mechi nyingine moja tu, United ikifungwa nyumbani na West Brom.
Hernandez amesema kwamba wakati akiwa ana furaha kuchezea klabu kubwa kama hiyo, pia anataka nafasi zaidi za kucheza na anaamini anaweza kuwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza iwe Old Trafford au katika klabu yoyote.
Looking ahead: Javier Hernandez in action during training with the Mexico squad this week
Anaangalia mbele: Javier Hernandez akiwa mazoezini na kikosi cha timu yake ya taifa ya Mexico wiki hii
Looking ahead: Javier Hernandez in action during training with the Mexico squad this week
Looking ahead: Javier Hernandez in action during training with the Mexico squad this week
Relaxed: Hernandez chats with team-mates Oribe Peralta (left) and Javier Aquino (right) in Mexico City
Utulivu: Hernandez akizungumza na wachezaji wenzake, Oribe Peralta (kushoto) na Javier Aquino (kulia) mjini Mexico City

"Nasotea hiyo [kuanza katika mechi zaidi],"alisema Hernandez akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Mexico, Deportes Telemundo.
"Nafanyia kazi hilo- kupata nafasi kikosi cha kwanza. Nafahamu kwamba kiwango changu uwanjani kitaniruhusu kutimiza lengo hilo siku fulani, aidha hapa [Manchester] au popote katika klabu yoyote.
"Naelekea kutimiza miaka minne hapa [Manchester United] na kweli, kama ambavyo wakati wote nimesema, nina furaha kuwa tayari nimechezea moja ya klabu bora duniani, nafanya vizuri kila siku kutafuta muda zaidi uwanjani,".
Predator: Chicharito scored the winner against United's old rivals Liverpool at Old Trafford last month
Shujaa: Chicharito alifunga bao la ushindi United ikiwafunga wapinzani wake wa jadi, Liverpool Uwanja wa Old Trafford mwezi uliopita
Predator: Chicharito scored the winner against United's old rivals Liverpool at Old Trafford last month
Denied: Hernandez failed to hit the target in his only other start this season, against West Brom
Alichemsha: Hernandez hakuweza kufunga katika mechi yake nyingine pekee aliyoanza msimu huu dhidi ya West Brom

"Nahitaji kupewa nafasi zaidi kuonyesha uwezo wangu, kwa sababu kati yetu sote tunataka kutoa mchango wetu ili hii timu ishinde ubingwa,".
Hernandez amekuwa akisotea namba kikosi cha kwanza United kutokana na kuzidiwa kete na akina Wayne Rooney, Robin van Persie na Danny Welbeck, lakini Mmexico huyo amesema hiyo inaweza kuwa nzuri kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu England.
"Ushindani ndani ya timu wakati wote umekuwa mkubwa na ninafikiri hiyo inaisaidia timu kwa kiasi kikubwa, kwa sababu kuna wachezaji wengi bora ambao kila mmoja kati yao anataka nafasi kikosi cha kwanza,".
"Mazoezi na mechi zinazokuja zitatulazimisha kusimama imara kuisaidia timu kuimarika kwa vyote, kwa uchezaji binafsi na kitimu kwa ujumla,".

Hivi Moyes anaweza kuwa 'chizi' kumruhusu Hernandez kuondoka? Hizi ni takwimu za washambuliaji wa United katika Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa, ambazo zinaonyesha ni mshambuliaji mkali zaidi United...
United's strikers
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari