Like Us On Facebook

MKE NA MUME WATUPWA LUPANGO , NI KWA SABABU YA ILE KESI YA EPA, SOMA HAPA

               WATUHUMIWA watatu kati ya watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamehukumiwa kifungo jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani ambapo kati yao ni mke na mume.

Mke na mue hao ni Manase Makale aliyetupwa jela miaka 5 na mkewe Eddah Makale aliyetupa jela miezi 18 sawa na mwaka mmoja na nusu Pamoja na Bahati Mahenge, aliyehukumiwa kifungo cha Miaka 7 lupango.
Mbali na hukumu hiyo washitakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya wizi wa Sh1.86 bilioni za EPA, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kupitia Kampuni ya Changanyikeni Residential Complex wametakiwa kulipa fedha kiasi cha Sh 1.5 Bilioni.
Washitakiwa wawili wameachiwa huru na Mahakama hiyo baada ya Mahakama kushindwa kuwatia hatiani.

CHANZO FATHER KIDEVU BLOG
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari