Like Us On Facebook

AUNT EZEKIEL ACHENGA KUANDAMWA NA MIKOSI!

                                                                Aunt Ezekiel.
 STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema hana mkosi kama watu wasiomtakia mema wanavyoeneza maneno mitaani
Akipiga stori na paparazi wa Ijumaa juzikati, Aunt alisema kuna baadhi ya watu wasioitakia mema ndoa yake wamekuwa wakieneza maneno kwamba ana mkosi ndiyo maana kila mwanaume anayekuwa naye hupatwa na balaa.
Staa huyo aliongeza kuwa haumizwi kichwa na maneno hayo kwa kuwa anaamini kila kinachotokea katika maisha yake ni mipango ya Mungu.
“Maneno yao ni imani potofu na siwezi kumfikiria mwanaume niliyewahi kuwa naye huko nyuma kabla ya kuolewa na mume wangu Demonte kwani hakuna baya lililomfika tangu tulipooana,” alisema Aunt.

-GPL
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari