Rehema Chalamila maarufu kama Ray C alikaa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki na pia kupitia mambo mengi sana, kitu kizuri hivi sasa amesharudia hali yake ya zamani na yuko tayari kurudi kwenye muziki. Kupitia XXL ya Clouds FM aliongea na B12 kuhusu mpango wa ujio wake mpya. Soma hapa interview yote ilivyoenda na sikiliza hapo chini sauti yake.
B12: Baada ya muda mrefu sana online niko live na mwanadada Ray to C, Ray C mambo vipi?
B12: Za siku?
RAY C: Salama namshukuru mungu sana.
B12: Naona umetoka chimbo?
RAY C:Niko fiti sana na nikaona niongee na nyinyi leo.
B12: Nimefurahi sana kuongea na wewe, uko fresh kabisa yani mzima kabisa?
RAY C: Mimi mzima kabisa Dozen mungu mkubwa.
B12:Yah mungu ni mkubwa,unajua watu kibao hawaamini kama naongea na Ray C ujue. Fanya kama unanipa ile ya zamani basi.
RAY C:Ray C anaimba (Kama penzi langu nilikupaa loteeee)
B12: Rayc1982 kwenye Instagram right?
RAY C:Yap, Rayc1982 unanipata kwenye Instagram.
B12: Oky kwa watu wote ambao wanataka kuona picha za Ray C unaweza kwenda kuzicheki picha zake. Niambie game ya music ulivyokuwa unaisikiliza sasa hivi, unaweza kurudi uka-fit sehemu ambayo una-staili ku-fit.
RAY C: Inawezekana, dada yao si unajua niko fiti. Napenda kuona watoto wanafanya vizuri wakina Linah, Recho kadogo kangu hako kamenirithi. Nikisikiliza kazi zake kizunguzungu naona game iko tight. Nikirudi lazima nishirikiane na wanangu.
B12:Kuna vitu ambavyo nilitaka kuzungumza na wewe sema nimeskia wiki ijayo utafanya press conference kuhusu ujio wako.
RAY C:Yah ni kweli, nimeona mambo ya ma-instagram, facebook naongea na mashabiki wangu sana.Wengi wananiuliza when are you coming back, we miss you nini na vitu kama hivyo. Nikaona niongee na wewe kwamba next week narudi mzimamzima, watasikia kazi zangu interview na Ray C mpya anakuja kivingine vizuri zaidi.
B12:Nambie uli-miss nini sana Ray C
RAY C:Nime-miss sana mashabiki wangu aisee, nimemiss sana muziki. Unajua muziki is my life yani acha kabisa, kwasababu kuna vitu vingi nimeviandika natamani sana watu wangu wasikilize.Muda mrefu sana tangu niko Nairobi na mambo mengine yakatokea lakini nashukuru nimerudi kwenye hali ya kawaida.Vitu ambavyo nimemiss ni vingi sema naskiliza watu kama Diamond, kusema kweli watoto ni wazuri.
B12:Mimi kama shabiki wako Ray C nime-miss sana vile viuno pale kwenye stage
RAY C:Nimenongesha(nimenenepa) kidogo, mashabiki wanaangalia kwenye Instagram hawaamini kama ndiyo mimi. Sema nafanya mazoezi nitarudi kwenye hali ya kawaida.
B12: Mwisho kabisa una maneno gani ya kusema kwenda kwa mashabiki zako au watu waliokusupport.
RAY C:Mimi ningependa kuwashukuru sana mashabiki wangu, support waliyonipa wakati naumwa. Nimepokea meseji nzuri sana wakati naumwa na watu wavumilivu kwa kweli. Naahidi kwamba Ray C huyu sio Ray C yule wa kipindi kile, mungu ni mkubwa na amenipendelea sana. Wakae tayari kupata kazi mpya kutoka kwangu.