MAGARI YAKIPITA KWA SHIDA BAADA YA AJALI HIYO
HAWAKOMI!WANANCHI WAKICHOTA BILA HOFU MAFUTA BAADA YA AJALI HIYO
Ajali hiyo ilitokea jana ambapo watu wawili wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.