Like Us On Facebook

KHADIJA KOPA: BAADA YA KUFIWA NA MUME WANGU NIMEBAINI KUWA NAPENDWA

                                                                  KHADIJA KOPA
Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Kopa amesema baada ya kufiwa na mumewe kipenzi, Jafari Ally, amegundua kuwa anapendwa na watu wengi tofauti na alivyokuwa akifikiria.
Akistorisha na mwandishi wetu, Khadija alisema kuwa kipindi alipokuwa kwenye matatizo alishangazwa na ukaribu ulioonyweshwa na watu hata ambao hakuwatarajia na ameijua nafasi yake kwenye jamii.
 “Nimesaidiwa na asasi mbalimbali, vikundi pamoja na watu wengi, huku wengine wakiniambia kuwa nikitaka msaada niwapigie ingawa sijafanya hivyo, nimefarijika sana kuona napendwa kiasi hiki,” alisema mwanamama huyo ambaye anatarajia kumaliza eda Oktoba 16, mwaka huu kabla ya kurejea mzigoni.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari