Like Us On Facebook

DEREVA ANASWA AKINGONOKA NDANI YA GARI LA KAMPUNI,POLISI WAMBANA!


Yelewiii!  Dereva ‘suka’ wa kampuni moja binafsi yenye makao yake makuu Kurasini jijini Dar (jina halikupatikana) Jumapili iliyopita alinaswa akifanya mapenzi na changudoa  ndani ya gari la kampuni hiyo, kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilishuhudia tukio hilo laivu.

Dereva huyo akiwa na mwenzake walifika maeneo ya Mbagala Zakhem saa 7 usiku wa Februari 16, mwaka huu bila kujua kama OFM ilikuwa katika maeneo hayo kwa ajili ya kufanya oparesheni tokomeza machangudoa.
OFM ilimshuhudia dereva huyo na mwenzake wakishuka ndani ya gari aina ya Toyota Hilux (isiyokuwa na ‘pleti’ namba upande wa  mbele) mali ya kampuni  hiyo, wakiingia kwa fujo katika moja ya madanguro maarufu na kupaki gari  kisha wakashuka kuelekea kwenye danguro la machangudoa.
Baada ya muda, mmoja wao alirejea akiwa na changudoa maarufu kwa jina la Waluwalu na kujifungia ndani ya gari hilo.
Kama kawaida yake OFM iliwataarifu askari wa Kituo cha Kizuiani waliokuwa doria katika eneo hilo ambao kwa pamoja walilivamia gari na kumuamuru dereva  ashuke.
Hata hivyo, suka huyo alikuwa mbishi akaamua kufunga milango na kupandisha vioo ili asiweze kubughudhiwa na kile alichokuwa akikifanya ndani ya gari.
Askari waliokuwa na silaha wakalizunguka gari hilo na dereva huyo alipoona mambo yamekuwa magumu alifungua mlango na kutimua mbio lakini hakufika mbali kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na changudoa aliyekuwa naye.
Akizungumza kwa hofu dereva huyo alisema, yeye na mwenzake ni madereva wa kampuni... (jina tunalo) na walikuwa maeneo hayo kwa bahati mbaya na si kama walifika kuwanunua machangu hao.
Dereva huyo alipotakiwa atoe sababu za kujifungia ndani ya gari hilo na changudoa kisha kutoa pleti namba ya mbele ya gari, alijitetea kwa kusema kuwa pleti namba ilidondoka barabarani tangu mchana, hivyo walikuwa wakimtafuta fundi ili awatengenezee.
Alipohojiwa changudoa waliyekuwa naye, hakuwa na lolote la kusema zaidi ya kuangua kilio na kuomba aachiwe huku akilaumu ukali wa maisha kama sababu ya kujiingiza katika biashara ya kujiuza.
Wahusika hao walifikishwa Kituo cha Polisi cha Kizuiani kabla ya kesho yake (Jumatatu) kupelekwa Mahakama ya Jiji kusomewa makosa yanayowakabili.
-GPL

KESI YA KIFO CHA KANUMBA... LULU AANIKA UKWELI,MAMA KANUMBA AMWAGA MACHOZI!!

MWANGA umeanza kuonekana juu ya kesi inayomkabili staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia staa mwenzake wa muvi, Steven Charles Meshack Kusekwa Kanumba ambapo safari hii aliamua kukiri vipengele kibao, Risasi Mchanganyiko lina habari yote.
Elizabeth Michael 'Lulu' aliyeambatana na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ wakiwa eneo la mahakama.
Akikiri mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania juzi (Jumatatu) wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, nyota huyo aliweka wazi mambo ambayo hapo awali hakuwahi kuyakubali kortini jambo lililovuta hisia za wasikilizaji waliokuwa wamefurika ndani ya chombo hicho cha kutoa haki kujua kinachoendelea.
Mwendesha mashitaka wa upande wa serikali, Monica Mbogo alivitaja vipengele kadhaa ambavyo Lulu alitakiwa kuvikana au kuvikubali.
Lulu, mama yake mzazi Lucresia Karugila wakiongea na mwanasheria wao, Peter Kibatala mahakamani.
Katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa ustadi mkubwa wa wanasheria kuoneshana ujuzi wa kusoma na ‘kubugia’ vipengele vigumu vya sheria, Lulu alipata wakati mgumu wa mambo kiasi cha kumwita wakili wake, Peter Kibatala mara kwa mara.
MADAI YA KUMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA
Lulu alikiri kwamba, mashitaka yake mahakamani hapo yalikuwa ya kumuua bila kukusudia, marehemu Steven Kanumba Aprili 7, mwaka 2012.

Lulu akiongea na mama yake kabla kesi yake kuanza kusikilizwa.
KUWEPO ENEO LA TUKIO NA KUTOKEA KWA UGOMVI
Katika maelezo yake, Lulu aliweka bayana kuwa siku ya tukio alifika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza ya Vatican jijini Dar saa 6 usiku na kuingia moja kwa moja chumbani.
Alizidi ‘kuchezesha taya’ kuwa, kulitokea ugomvi kati yake na marehemu licha ya kutotaja chanzo cha ugomvi huo.

Aliongeza kwamba, Kanumba alimvuta mkono na kumrudisha ndani wakati alipokuwa akijaribu kukimbia na kuufunga mlango, mwishowe alifanikiwa kutoka na kukimbia kusikojulikana.
KUKAMATWA KWAKE BAMAGA
Lulu aliweka wazi kuwa, siku ya tukio, saa 11alfajiri alikamatwa maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam alipokuwa akijaribu kutorokea kusikojulikana.

KUHUSU UHUSIANO
Bila kupepesa macho wala kuchezesha kope, Lulu alikubali kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Kanumba kwa muda ambao hakuutaja hali ambayo baadhi ya watu walionesha kuwa ‘sapraizidi’.

AMWAGA MACHOZI KORTINI
Awali, Lulu alipofika mahakamani hapo akiwa ameongozana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na staa wa muvi za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ alionekana kuwa na amani.

Msanii huyo alimudu kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo liliingia mtaani siku hiyo. Lakini baada ya kuanza kwa kesi, ilifika mahali alidondosha machozi hali iliyomlazimu kujifuta uso kwa kitambaa.
Baadhi ya watu walinong’ona kuwa, mrembo huyo alikuwa analizwa na kumbukumbu za tukio la kifo cha Kanumba na kwa sababu ya kuogopa kesi.

MAMA KANUMBA ASUSA
Habari nyingine zilidai kuwa, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa hakutokea mahakamani hapo licha ya umoja na udugu alionao kwa sasa na familia ya  Lulu.

Ilidaiwa kuwa sababu kubwa ya kushindwa kufika kortini ni kukosa uamuzi wa upande gani angekaa kati ya mshtakiwa (Lulu) na mshitaki (Jamhuri) kwa vile kote kuna muhusu kwa sasa.
“Unajua mama Kanumba alipogundua kwamba anayetakiwa kujibu madai ni Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu alimtangaza ni mwanaye na anayelalamika ni serikali, alishindwa kujua akija leo (juzi) angekaa upande gani? Akaamua kutokufika kabisa,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka kwa simu mama huyo lakini bila mafanikio kufuatia simu yake ya mkononi kuita muda mrefu bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Lulu alikamatwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa galacha wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba mnamo Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza Vatican jijini Dar.

Baada ya kukamatwa na kuswekwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar, Lulu alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo hakutakiwa kujibu ndiyo au hapana.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya madai hayo.
Aliachiwa kwa dhamana Januari 29, 2013 na kuambiwa kwamba kesi yake itakaporudi, itakuwa chini ya mahakama kuu. Juzi ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza.

-GPL

MUSWAADA WA KUPINGA USHOGA KUSAINIWA UGANDA.

ug_e861f.jpg
 
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema atasaini muswaada tata unaopinga ushoga na kuwa sheria kamili.
 
Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni onyo kwa wanaotetea vitendo vya mahusiano ya jinsia moja kuwa watashughulikiwa vikali nchini humo.
 
Mwezi uliopita kiongozi huyo alipanga kuachana na muswaada huo ambao umekuwa ukikosolewa vikali na wahisani kutoka mataifa ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binaadamu tangu ulipowasilishwa mwaka 2009. Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika mataifa ya Afrika na kinyume cha sheria kwa mataifa 37.
 
Wasiwasi wa mashoga wa Afrika
Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema Waafrika wachache waliojitangaza kuwa mashoga, wanahofu ya kufungwa, kukabiliwa na vurugu na kupoteza ajira zao.

Wakati wa mkutano wake na chama tawala nchini Uganda NRM kundi la wanasayasi liliwasilisha utafiti wao kuhusu mapenzi ya jinsia moja kwa rais Museveni. Msemaji wa mkutano huo, wa NRA Anite Evelyn katika taarifa yake alisema kuwa "Museveni alitangaza atasaini muswaada huo kwa vile swali lile la iwapo mtu anaweza kuzaliwa shoga au hapana limejibiwa".
 
Uchunguzi wa mawaziri
Katika taarifa yake kamati ya mawaziri iliyokuwa ikilifanyia uchunguzi suala hilo ilisema Ijumaa (14.02.2014) hakuna vinasaba vya mapenzi ya jinsia moja na kwa hivyo si ugonjwa lakini ni tabia isiyo ya kawaida ambapo mtu anaweza kujifunza tu kwa kupitia uzoefu katika maisha.
 
Katika mkutano na chama tawala cha NRM, Mshauri wa Rais katika masuala ya Kisayansi, Dokta Richard Tushemereirwe alimwambia kwamba "mapenzi ya jinsia moja yana athari kubwa kwa afya za watu kwa hivyo si jambo la kuachwa liendelee hata kidogo".
 
Muswaada wa kupinga uhusiano wa jinsia moja uliwasilishwa bungeni mwaka 2009, ambapo awali ulikuwa ukipendekeza adhabu ya kifo kwa wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinisia moja, lakini ukafanyiwa marekebisho kwa kuweka adhabu ya vifungo vya awamu gerezani na maisha kwa kile kilichotajwa kuwa mapenzi ya jinsia moja ya kuchochewa.
 
Rais Museveni alisisitiza kuwa , wahamasishaji, wanaojionesha na wote wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinsia moja kwa sababu za ukaidi wa kutumwa , hawatavumiliwa na watakabiliwa vikali.
Chanzo, dw.de/swahili

JUMA NATURE AKANUSHA UVUMI KUWA KAMPONDA DIAMOND KWENYE WIMBO WAKE MPYAA,MSIKILIZE NATURE AKITOLEA UFAFANUZI JAMBO HILO

Hatimaye Juma Nature, amezungumzia utata ulioibuka kwenye wimbo wake mpya Kama Jana, unaohusiana na kama kweli amemdiss Diamond.
Akiongea na kipindi cha Showtime Next Chapter, Juma Nature aka Kiroboto amesema jina la ‘Dada Mondi’ lililofanya wengi waamini kuwa ni version yake ya Diamond, ni jina la msanii mwingine kabisa. “Hamna diss ya kumdiss Diamond, Diamond hajadisiwa,” amesema Nature. “Pale katajwa mtu mwingine kabisa anaitwa Dada Mondi na anakaa mitaa ya kwetu. Bado hajatoka halafu anataka sifa.”
nature
Msikilize hapo chini.

 

HUYU NDO MZUNGU ANAYEFANYA BIASHARA YA BODABODA JIJI DAR,MTAZAME HAPA!



Hapa Mzungu huyo akiwa kijiweni maeneo ya Bamaga akisuburi wateja

AIBU:DIVA WA CLOUDS APEWA MAKAVU LIVE KUHUSU "MATAKO YAKE YA BANDIA

Huddah kushoto na Diva kulia..
Diva Loveness Love apewa maneno mazito na matusi kutoka kwa mashabiki wanaomfatilia katika kazi zake za hapa na pale. katika kauli hiyo shabiki huyo alifunguka na kumjadili Diva vya kutosha
 

Nanukuu "Huyu diva hivi ana akili kweli kudanganya watu kweupe ndio nini ... Embu angalieni hiyo picha ndio mtaelewa Yani Kabisa milima na mabonde kuvaa godoro ndio ili iweje ... Diva acha ujinga unachekwa mjini kwa kutafuta tako kinguvu acha kuvaa maana shape inajulikana ni Ya simba,, cha ajabu ukikutana nae hayupo hivyo kabisaaaaaaa...
 Na camera 360 acha kabisa unajipimp sana wakati We ni mbaya kuvaa malenz mwisho utapata macancer Ya macho Bure... ... Swala ni kuacha kuvaa matako bandia usishindane na hudda mwenzio kaajaliwa"

BAADA YA KUTANGAZA KURUDI SHULE,CHEKA AANZA UTORO SHULENI!

Bondia Francis ‘SMG’ Cheka, amedaiwa kuingia darasani siku moja tu tangu aliposajiliwa kama mwanafunzi mpya wa Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro Septemba mwaka jana.
Akizungumza na MWANANCHI, mwalimu wa Cheka aitwaye Mkisi amesema Cheka ameomba kuendelea na masomo baada ya kutoonekana darasani kwa miezi kadhaa bila taarifa yoyote, na kubainisha kuwa hawawezi kumruhusu kuingia muhula wa pili.
Cheka alipewa ufadhili wa masomo chuoni hapo mwaka jana mara baada ya kutwaa ubingwa wa dunia wa WBF Agosti 30, baada ya kumpiga Phil Williams wa Marekani katika pambano lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkisi amesema kuwa bondia huyo amekosa vipindi kwa muda mrefu hivyo hawezi kuingia muhula mwingine, kwakuwa atakosa vitu vingi hivyo anapaswa kujisajili kama mwanafunzi wa muhula mpya utakaoanza Machi 24.
“Cheka aliingia darasani siku moja na ‘kupotea’ hata hivyo hivi karibuni alikuja na kutuambia anataka kuendelea na shule ingawa hatuwezi kumuendelezea programu yake ya awali,” alisema Mkisi.
-Mwananchi

WAKUBWA TUU: MANENO YA KUPANDISHANA "NY*GE" KWA WANANDOA/WAPENZI!



Inawezekana wengi wetu tukawa tunayatumia bila kujua kwamba tumekusidia kuyatumia. Haya ni maneno au kauli ambazo mume/mke anaweza mwambia mwenza wake kama ishara ya kumpandisha "ny#ge"kabla ya kuanza kufanya map3nzi. Wawili hawa wanaweza wakawa sehemu tofauti tofauti, mfano mume yupo kazini lakini anakaribia kurudi nyumbani, mke ukaanza "kumcharura" mumeo kwa kauli mbali mbali aidha kupitia sms au kwa kumpigia simu, ingawa kupitia sms ndo inasisimua zaidi!
               -
Hapa najua naongea na watu wazima, sina haja ya kuandika zaidi maneno yenyewe lakini kila mmoja ni mjuzi wa tabia na vitu ambavyo mwenza wake anavihusudu hasa mkiwa kitandani, mfano" Baby ukirudi leo nataka unipindishe pale katika dressing table kama ulivyonifanyia jana, na leo nimevaa lile gauni ulipendalo na zile bikini mpya, dont be late my l0ve" Maneno haya kwa anayejua mapenzi na anampenda mkewe ni lazima huko alipo "Jogoo" awike kidogo! nayeye hawezi kubaki kimya lazima atajibu mashambulizi, nna uhakika itafikia point kila mtu, Udenda Utamtoka kwa nafasi yake.......! Na kila mmoja akawa na hamu ya map#nzi na mwenzie! Tuyatumie Maneno hayo kwa nafasi zetu! Yanahusika saaana!  ADIOS!!!!

SAMAHANI KWA PICHA HIZI..........BUT NDIYO MAISHA YA WANAFUNZI MAHOSTELI.....

NI AIBU KUYAGEUZA MAISHA YA SHULE KUWA KAMBI YA MAPENZI

Siku hizi ni kawaida kwa wanafunzi kupiga picha chafu kwa kisingizio cha ugumu wa maisha.......

Mbali na kisingizio hicho, wapo pia ambao hupiga kwa lengo la kutafuta umaarufu na wapo pia ambao hupigwa na wapenzi wao pasipo kukusudia........

Haijalisha alipigwa na mpenzi wake au alijipiga bila kukusudia.Sote tunajua,mwanafunzi ni sawa na kioo cha jamii maana hao ndo viongozi wa taifa la kesho.....Iko haja ya kubadilika

LAAANA!! CHEKI WANAFUNZI WA KIKE WAKINYONYANA MATE MCHANA KWEUPE

Hawa ni wanafunzi wakiwa katika pozi la kushangaze watu,kwa kitendo cha kula mate (kubadilishana ndimi zao) tena mbele ya wanaume je tunaelekea wapi? Toa maoni yako ..Nini Kifanyike kuwasaidia mabinti hawa walio tokwa na maadili ukichukulia tabia hii inazidi kuongezeka siku hadi siku miongoni mwa dada zetu

LOWASSA NA WENZAKE SITA WAPEWA ONYO KALI NA CCM

Press Conference ya CCM imefanywa na Nape saa 8.... Issue ni kwamba wale vigogo 6 wa CCM wamepewa onyo kali, karipio na kwa maana hiyo watakuwa chini ya uangalizi maalumu kwa miezi 12 kuanzia jana kutogombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya CCM... Lowassa, Ngeleja, Membe, Wasira, Januari, Sumaye... Uwezekano wa kugombea nafasi ya urais yaota mbawa?
-udaku special

DIAMOND NA D'BANJ KUJA NA MAMBO MENGINE, YASOME HAPA mambo hayo!


pichani ni Diamond Platnumz na D' BANJ wakiwa studio ready kutengeneza muziki mpya, sasa Diamond kutoa nyimbo nyingine na D'BANJ..Diamond alipost hiyo picha na kuandika maneno haya hapa chini...

Busy day....Studio session with King D'Banj... Cc @iambangalee

MCHAWI WA UNGO ADONDOKA, AGEUKA KUKU


HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji  la  Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika  kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo, Uwazi limeona mengi.

Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.

“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo  mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.

Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha.

MHHH HATARI: UTAJIRI WA MBUNGE WA CCM "VICKY KAMATA" NI BALAA..KANUNUA HADI MGODI,CHEKI MWENYEWE HAPA


WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele…yelele… Hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata anayetajwa kuwa na utajiri balaa.


Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata.
UWAZI LINA KILA KITU
Vicky amepata mafanikio makubwa ambayo kila mwanamke Tanzania angependa kuyapata. Gazeti hili lilimchimba kwa kina na kupata utajiri wote alionao kwa sasa.

KABLA YA SIASA, KABLA YA BONGO FLEVA
Kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania waliozaliwa katika familia duni.
Katika kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, Vicky amewahi kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva na kutunga nyimbo mbalimbali, wimbo wa Wanawake na Maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika jamii.

“Nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda Morogoro.
“Kila kitu kinabadilika kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky mwenye watoto wawili, Revocatus na Glory (jina la baba halikutajwa).
MAFANIKIO YAANZA
Mwaka 2006, Vicky alifanikiwa kuajiriwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akiwa ni afisa uhusiano.
Mwaka 2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita.

MJENGO WA GHOROFA MBILI
Akiwa mbunge, Mheshimiwa Vicky ameingia kwenye orodha ya wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili Sinza jijini Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne.

Ndani ya ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea ‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia yake.
MAGARI YAKE SASA
Kama walivyo matajiri wengine, mheshimiwa huyo anamiliki magari manne ya kifahari, yote yakiwa na thamani ya shilingi milioni 261.
Ana Toyota Voxy- Noah ambalo alilitoa sokoni kwa shilingi milioni 16.
Kamata pia anamiliki BMW X5 likiwa na thamani ya shilingi milioni 130.

Mara nyingi anapokwenda bungeni, Vicky hutembelea gari linalomudu mikiki ya barabarani, Toyota Land Cruiser ‘VX’ ambalo lina thamani ya shilingi milioni 90.
Pia mwanamama huyo ana gari aina ya Toyota Altezza alilolinunua kwa shilingi milioni 25.

ANAMILIKI MGODI WA DHAHABU
Wakati hayo yakiwa wazi, chanzo makini kilidai kuwa, mheshimiwa huyo amenunua mgodi wa dhahabu Geita, jambo ambalo ni sehemu kubwa ya mafanikio yake.

“Vicky amenunua mgodi wa dhahabu Geita, mimi ni mtu wangu  wa karibu, hapendi kusema mafanikio yake wala watu wajue lakini ukweli ndiyo huo. Eneo ni kubwa, muda si mrefu uchimbaji utaanza,” kilisema chanzo cha habari kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
ANA SHAMBA LA EKARI 157
Utajiri wa mheshimiwa huyo unaendelea kuanikwa kuwa, ni pamoja na shamba  lenye ekari 150, Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Pia ana shamba la miti Kibamba, Dar lenye ekari 7.

NI MFUGAJI
Mbali na mambo mengine, Vicky ni mfugaji kama ilivyo asili ya Wasukuma. Anafuga ndege aina ya kanga, kuku wa kisasa na mbuzi.

ANASOMESHA WATOTO WASIOJIWEZA
Katika mambo ambayo huenda yanachangia kuchota baraka, mheshimiwa Vicky anawalipia ada ya sekondari watoto yatima, walemavu na wasiojiweza kimaisha, idadi yao ikifikia 75.

KIPATO CHAKE KIKOJE?
Dodoso zinaonesha kwamba, kwa kazi ya uheshimiwa, kwa mwezi anaingiza shilingi milioni 15 ukijumlisha posho zote za ubunge, ujumbe wa kamati ya bunge na mshahara.

AMFUNIKA ANNE MAKINDA
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, jumba la kifahari la Vicky Kamata linalifunika lile la bosi wake ambaye ni spika wa bunge, mheshimiwa Anne Makinda. Yeye nyumba yake ipo Kijitonyama.

ULINZI NYUMBANI KWAKE USIPIME
Uwazi lilipata bahati ya kufika nyumbani kwa Vicky  na kukumbana na ulinzi wa mitambo ya kisasa ya kuzuia wezi na majambazi kwa saa 24.
Ili mgeni aingie ndani ya geti huhojiwa na walinzi kwa dakika zisizopungua kumi.

WABAYA WAKE WAMUUNDIA ZENGWE LA FREEMASON
Huwezi kupendwa na kila mtu, hii ni baada ya mwandishi wa gazeti hili kuamua kupiga kambi kwa muda wa siku mbili jirani na nyumba ya mheshimiwa huyo ambapo baadhi ya watu waliohojiwa kuhusu ukwasi wa mbunge huyo mwanamke walisema huenda ni memba wa Freemason.

“Mafanikio ya mbunge huyu bwana ni makubwa mno, tunasikia watu wakisema huenda ni Freemason. Lakini ndivyo tulivyo Watanzania, mtu akifanikiwa kidogo wanasema ni Freemason, ninavyomfahamu huyu dada amepiga hatua, sijawahi kumsikia na mambo ya Freemason,” alisema jirani mmoja na kuungwa mkono na wenzake.
MSIKILIZE VICKY
Katika mahojiano maalum na Uwazi kuhusu utajiri wake, Vicky alisema:
“Mafanikio yote yametokana na juhudi zangu za kujituma katika kufanya kazi, namwamini Mungu siku zote. Hakuna dhambi mbaya hapa duniani kama kukata tamaa.

“Tukifanya kazi kwa kujituma na kumwamini Mungu hakuna Mtanzania maskini.
“Kila mtu ana uwezo wa kubadilisha mfumo wa maisha akiamua, umaskini wa watu si chaguo la Mungu, kila jambo litokealo kwa mwanadamu lina maana kubwa kwa Mungu.”

KAULI YA UWAZI
Wanawake nchini waige mfano wa Vicky kwa kukamata fursa mbalimbali na wanapofanikiwa wawasaidie wengine, kama kusomesha yatima na wasiojiweza

ANAPENDA KUICHEZEA YANGU ILA KU DO HATAKI KABISA...!! MSAADA JAMANI NIMFANYEJE DEMU WA NAMNA HII...??


Kuna binti mmoja, nilikua nampenda sana, nkamtongoza akanambia hawez kuwa mpenzi wangu coz ana boy wake.. Tukawa marafiki,, siku moja akaniomba twende disko, tulipomaliza kucheza akasema nkalale kwake, nkajua nafasi ndio hii. Cha ajabu tulipolala hakutaka tufanye tendo ila aliniambia anapenda kuichezea yangu, nkamwachia achezee na mie nikawa nayachezea matt yake, tukachezeana hadi tulipopata usingizi. Ikawa ni tabia yake tukikaa pazuri tu lazima aichezee yangu na mie nachezea kifuani pake. 

KILA NIKIMUOMBA KUFANYA ALIKATAA. Hatukuwahi kula hata denda, alikua anakataa.
Sasa hivi niko mbali naye, anadai kamisi kuichezea.. Na kamuacha jamaa.. Nkimuuliza kuhusu ku-do anasema nisitegemee... Nkiendelea kuomba atanichukia.

Wataalamu niambie nini kifanyike hapo?

AIBU KUBWAA...!! MREMBO AFUMANIA PICHA ZA NUSU UCHI ZA RAFIKI YAKE KIPENZI KWENYE SIMU YA MCHUMBA WAKE..TAZAMA HAPA.


Ni siku ambayo sito isahau. Siku amini macho yangu siku nilipokuta picha za nusu uchi za rafiki yangu kipenzi Nancy kwenye simu ya mpenzi wangu Dany.
Picha zilitumwa watsapp na yeye mwenyewe Nancy kwenye simu ya mchumba angu.Nilipo muuliza alinijibu kwa ujasiri tu kwamba wamekuwa wakidate kwa muda sasa, na huku akiongezea kwamba Dany is so sweet yani huyo
mchumba angu. Daaah Nifanyaje jamani. Naombeni USHAURI..!!

MWANAFUNZI WA CHUO AJINYONGA BAADA YA KUFELI MITIHANI

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Ualimu  cha Winneba, nchini Ghana, amejiua kwa kujinyonga mara baada ya jina lake kubandikwa kwenye ubao wa matangazo (notice board) kuwa amefeli masomo matatu.



Jina la mwanafunzi huyo limehifadhiwa kwa sasa, ila inasemwa kuwa sababu ya kujinyoga kwake ni kutokana na kufeli masomo hayo matatu ambapo kungepelekea kufutwa kwake shule hapo.

Sababu hasa ya kifo chake haijajulikana moja kwa moja ila inaaminika ilitokana na hofu ya kutimuliwa chuoni hapo kutokana na kufeli mitihani mitatu.

Wilson Dabuo, ambaye ni muwakilishi wa wanafunzi kwenye baraza la chuo hicho, alieleza kupitia Joy News kwamba chuo hicho kina sheria ya kutimua wanafunzi wanaofeli masomo matatu kwenye mitihani yao.

HATARI POSHO ZA SERIKALINI: WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUVUNA MILIONI 21...TSH 300,000/ KWA SIKU

HATIMAYE serikali imeweka hadharani kwamba kila mjumbe katika Bunge la Katiba ataweka kibindoni posho ya sh 300,000 kwa siku.


Kwa maana hiyo, kila mjumbe katika Bunge hilo atakuwa amelipwa sh milioni 21 kwa siku 70 za uhai wa Bunge hilo, na kama serikali itaongeza siku 20 zaidi kwa mujibu wa katiba na kufikia siku 90, kila mjumbe atavuna sh milioni 27.


Awali gazeti hili liliwahi kuripoti majadiliano ya ndani serikalini kabla ya jana kuthibitishwa rasmi ambapo kulikuwa na pendekezo la kutaka kila mjumbe alipwe sh 700,000 kwa siku.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah, alisema kuwa kila mjumbe katika Bunge hilo atalipwa sh 300,000 kwa siku.

Alisema malipo ya wajumbe hao ni pamoja na posho zote za vikao ikiwa imeunganishwa na posho za madereva.

Pia alieleza kuwa gharama zote ambazo zimetumika katika matengenezo ya ukumbi na sehemu nyingine ni sh bilioni 8.2 na fedha hizo ni bajeti ya kawaida ambayo ilipitishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14.

Mbali na hilo, Kashililah alisema kuwa kutokana na umuhimu wa kuwepo kwa Bunge Maalumu la Katiba, Bunge limehakikisha linafanya ukarabati ikiwa ni pamoja na kufunga mitambo mbalimbali ya usalama na kurekebisha mifumo ya kiutendaji.

Alisema matengenezo yaliyofanyika ni pamoja na kurekebisha paa la jengo la ukumbi wa Bunge ambalo awali lilikuwa likivuja wakati wa mvua.

Akitoa ufafanuzi zaidi katika ufungaji wa viti ndani ya ukumbi wa Bunge hilo, alisema  kuna viti 678 na kurekebisha vipaza sauti ambapo kazi hiyo pekee imegharimu dola za Kimarekani milioni moja.

Kuhusu maandalizi, alisema yamekamilika na wajumbe wameishaanza kufika bungeni kwa ajili ya usajili.

Alisema vikao vya Bunge vitaanza  rasmi Februari 18 majira ya saa nane mchana na wataanza kwa kumchagua mwenyekiti na makanu wake.

Alisema ratiba ya Bunge la Katiba itaanza na mkutano wa maelekezo kwa wajumbe Februari 18 asubuhi na Bunge lenyewe litaanza siku hiyo hiyo saa nane mchana.

Kwa mujibu wa katibu huyo, shughuli nyingine zitakazofanyika ni pamoja na mwenyekiti wa muda kusimamia uandaaji  na upitishwaji wa kanuni.
Alisema mwenyekiti wa muda atasimamia uchaguzi wa mwenyekiti na baada ya kupatikana mwenyekiti na makamu wake, ndipo atakapopatikana katibu ambao wataapishwa na Rais Jakaya Kikwete.
Uhai wa Bunge hilo utakoma Aprili 30 au kwa ridhaa ya rais.
-Tanzania Daima

MODEL WA TANZANIA HAMISA AZUNGUMZIA KUTOA PENZI KWA MWANAMUZI DIAMOND...HUYU HAPA

MREMBO anayedaiwa kuliingilia penzi la staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania, Amisa Mabeto amefunguka kuwa  mwanamuziki huyo ni shemeji yake tu, hakuna chochote kati yao.
Amisa Mabeto.
Akipiga stori na safu hii kuhusiana na madai hayo, Amisa alisema alistaajabu kwani hana mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi kuonana miaka ya nyuma, tena siyo kimapenzi.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa, siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu,” alisema Amisa.
Amisa aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano na Diamond akiwa ni shosti mkubwa wa Wema.

LULU AKUMBUKA MAPENZI YA KANUMBA VALENTINE’S DAY

WAKATI kesi yake juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba ikianza kurindima leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa la moyoni akikumbuka mapenzi ya jamaa huyo aliyetangulia mbele za haki.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa iliyopita.
 
Marehemu Steven Kanumba.
“Kuna mtu natamani kumtakia Happy Valentine’s Day kwa kuwa nakumbuka mapenzi yake kwangu lakini kwa bahati mbaya siwezi kwa sababu hayupo na haiwezekani tena,” alisema Lulu.
Hata hivyo, alipobanwa amtaje, staa huyo ambaye ni sura ya mauzo ya filamu za Kibongo alikiri kuwa ni Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012, siku ambayo kamwe hawezi kuisahau maishani mwake.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari