UCHUMBA wa staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mpenzi wake anayefahamika kwa jina moja la Siwema umedaiwa kuvunjika.
Kwa mujibu wa chanzo makini, chanzo cha kumwagana ni baada ya Siwema
kukuta meseji za watoto wa kike tofauti katika simu ya Nay wa Mitego
katika nyakati tofauti.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, wawili hao walimwagana tangu Januari 2,
mwaka huu, nyumbani kwa Nay wa Mitego, Manzese jijini Dar es Salaam
baada ya Siwema kujiridhisha kuwa mpenzi wake huyo anamsaliti kutokana
na ushahidi wa meseji alizozifuma.
Hata hivyo, chanzo kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wapendanao hao
wamekuwa wakizinguana mara kwa mara na kilichomuuma zaidi Siwema ni
baada ya mkali huyo kuachia video yake mpya ya Nakula Ujana ambayo
ameonekana katika pozi za kimahaba na warembo kibao.
“Imemuuma sana video ya Nakula Ujana, warembo wale inasemekana
hakuishia katika video, sasa aliendelea kuwasiliana nao na Siwema
akagundua ndipo mtiti ulipoibuka, Siwema akarudi kwao Mwanza,” kilisema
chanzo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Siwema
ambaye alikiri kugombana na Nay na kusema ameshindwa kuvumilia na ameona
ili kujiepusha na presha zisizo za lazima arudi kwao Mwanza.
“Kweli tuna ugomvi na Nay na haswa kuna mambo yananikera sana ila
kubwa zaidi kwa sasa ni ile video yake mpya kuna parties mle
sijazipenda...mchumba wa mtu ufanye video ujiachie vile, unashikwa
shikwa ovyo,” alisema Siwema.
Alipotafutwa Nay, alikiri kutokea kwa ugomvi huo na kudai yupo katika
jitihada ya kumaliza tofauti hizo kwa kuzungumza na Siwema.