“Kwanini kanidiss huyo mtoto,” Chidi alisema.
“Design yake kumbe hii, manondonondo, naye mhuni Manzese, na mimi ni Chidi najulikana kwa story za kihuni, kwahiyo mpaka dakika hii amenidiss, either maskani yao ashajipanga. Mbili kashajua kwamba siku tukikutana kwenye show ‘labda Chidi akitaka kuniletea noma, na mimi nasimama nioneshe watu kuwa mimi huniwezi wewe’. Tatu kanizingua kuna mtu ana mchongo wake katika huu muziki kazinguana na mimi kalichukua ‘hilo toto’ kaliambia ‘fanya hivi na hivi, imba sauti kama… fanya hivi beba manondo, tembea kifua wazi ile kama mimi.. eeh unakuwa..halafu tukana jamaa’. Ni mchongo wake kwahiyo hata kama mimi nikibishana ‘nalo’ vipi kuna mtu mchongo wake yeye anachukua hela.”